
Nafasi za kazi Unitrans Tanzania, Unitrans Limited inakaribisha maombi kutoka kwa waombaji waliokidhi vigezo na wenye ujuzi kwa ajili ya kujaza nafasi zifuatazo:
Kampuni ya Unitrans Tanzania inakaribisha maombi kutoka kwa waombaji wenye sifa na ujuzi stahiki kujaza nafasi zifuatazo:
1. Dereva wa lori (Nafasi 70)
Eneo la kazi: Kilombero
Aina ya mkataba: Msimu
Majukumu:
- Kufanya kazi ya kusomba miwa kutoka mashambani kwenda kiwandani
- Majukumu mengine yanayoendana na taaluma ya udereva
Sifa za mwombaji:
- Awe na ufahamu wa Sheria ya Usalama Barabarani na kanuni zake
- Awe na leseni halali ya daraja E
- Awe anajua kusoma na kuandika
- Awe na cheti halali cha mafunzo ya udereva kutoka chuo kinachotambulika na serikali. Wenye cheti cha daraja la pili (Advanced Drivers Grade II – Industrial) watapewa kipaumbele
- Awe na uzoefu wa kuendesha lori usiopungua miaka 3
- Awe na umri usiopungua miaka 25 na usiozidi miaka 45
- Awe tayari kufanya kazi usiku
- Awe na barua ya vithibiti vya leseni kutoka jeshi la polisi Tanzania
Jinsi ya kutuma maombi: Nafasi za kazi Unitrans Tanzania
Maombi yote yatumwe kwa Meneja Rasilimali Watu, Unitrans Tanzania Ltd, P.O. Box 50, Kidatu. Waombaji wote wanatakiwa kuambatisha barua ya maombi, wasifu binafsi (CV), nakala za vyeti, nakala ya cheti cha mafunzo ya mlipa kodi (TIN number certificate), nakala ya kitambulisho cha NIDA kupitia barua pepe: [email protected]
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17 Juni 2025.
Angalia Hapa: Jinsi ya Kujisajili na Ajira Portal
Be the first to comment