
Fursa ya Kujiunga na Vyuo vya Diploma vya NACTVET 2025/2026, Kama wewe ni mhitimu wa Kidato cha Nne au Kidato cha Sita na unataka kuendelea na elimu ya juu, huu ndio wakati wako! Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limefungua rasmi udahili kwa mwaka wa masomo 2025/2026 katika vyuo vya diploma na astashahada nchini.
Hii ni nafasi ya kipekee ya kuchagua chuo unachokitamani na kujiunga na kozi unayopenda. Lakini kumbuka, muda wa kutuma maombi unakaribia kuisha—usiache hadi dakika za mwisho!
NACTVET Inatoa Kozi Gani?
Kupitia vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET, unaweza kusoma kozi mbalimbali zinazokupa ujuzi wa vitendo na maarifa muhimu kwa ajira au kujiajiri. Baadhi ya fani zinazopatikana ni:
- Uhandisi
- Teknolojia
- Kilimo
- Biashara
- Sayansi ya afya (kupitia mfumo maalum wa CAS)
Elimu hii ya ufundi stadi ni njia bora ya kujenga maisha yako kwa msingi imara wa maarifa na vitendo.
Faida za Fursa ya Kujiunga na Vyuo vya Diploma vya NACTVET
1. Ujuzi wa Vitendo: Unajifunza kwa kufanya – si tu kusoma vitabuni.
2. Fani Mbalimbali: Kuna chaguo nyingi kulingana na kipaji au ndoto zako.
3. Ajira au Kujiajiri: Wahitimu wengi hupata ajira haraka au huanzisha miradi yao ya kujitegemea.
4. Elimu Bora: Vyuo vya NACT VET vinatoa elimu ya kisasa inayoendana na mahitaji ya sasa ya soko la ajira.
Tarehe Muhimu za Udahili 2024/2025
📌 Mwisho wa kutuma maombi kwa kozi zisizo za afya na kozi zote za Zanzibar: 14 Julai, 2024
📌 Mwisho wa kutuma maombi kwa kozi za afya na sayansi shirikishi Tanzania Bara kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS): 30 Juni, 2024
Jinsi ya Kutuma Maombi
✅ Kozi zisizo za afya na zinazotolewa Zanzibar:
Tuma maombi moja kwa moja kwenye tovuti au ofisi za vyuo unavyotaka kujiunga navyo.
✅ Kozi za afya na sayansi shirikishi (Tanzania Bara):
Tuma maombi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaopatikana kwenye tovuti ya NACTVET:
🌐 www.nactvet.go.tz
Be the first to comment