Jinsi ya Kuangalia Salio NSSF, Programu ya NS SF Taarifa – Mobile App inakupa fursa ya kufuatilia michango yako, salio lako, na kupata huduma mbalimbali za NS SF kwa urahisi. Hapa tutakuelekeza jinsi ya kutumia programu hii pamoja na njia nyingine za kupata taarifa kuhusu michango yako.
Jinsi ya Kuangalia Salio NSSF
1. Kutumia NSSF Taarifa – Mobile App:
Hatua za Kuanza:
- Pakua Programu: Nenda kwenye Google Play Store na pakua programu ya NS SF Taarifa.
- Jaza Taarifa zako: Weka Membership ID (nambari ya mwanachama) inayopatikana kwenye kadi yako ya NS SF.
- Jisajili: Jaza taarifa zako na ujisajili kwa kutumia barua pepe na nenosiri utakalotengeneza.
- Ingia kwenye Akaunti yako: Tumia barua pepe na nenosiri ulilozungumzia ili kuingia kwenye programu.
- Angalia Michango: Bofya sehemu ya “Statements” ili kuona michango iliyowasilishwa na mwajiri wako kwenye Shirika la NS-SF.
2. Kutumia NSSF Taarifa – WhatsApp:
Njia nyingine rahisi ya kupata taarifa ni kwa kutumia huduma ya WhatsApp. Hapa chini ni maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hii:
Hatua za Kutumia WhatsApp:
- Save Namba Maalum: Hifadhi namba ya NS SF 0756140140 kwenye simu yako.
- Fungua WhatsApp: Fungua programu ya WhatsApp na tuma ujumbe wa salamu kama “Hello” au “Habari” kwa namba hii.
- Pokea Maelekezo: Utapokea ujumbe wa maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hii.
- Pata Taarifa:
- Tuma “Statement” ili kupata taarifa za michango yako yote.
- Tuma “Balance” ili kupata salio la michango yako.
3. Kutumia NS SF Taarifa – SMS:
Unaweza pia kupata taarifa zako za michango kupitia ujumbe mfupi (SMS). Fuata maelekezo haya:
Hatua za Kutumia SMS:
- Tuma Ujumbe: Ingia kwenye sehemu ya ujumbe (SMS) na tuma ujumbe kwenda namba 15200.
- Huduma za Salio/Balance: Tuma ujumbe wenye muundo huu:
NSSF SALIO (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)
- Au:
NSSF BALANCE (Member Number) (Year)
- Huduma za Taarifa/Statement: Tuma ujumbe huu:
NSSF TAARIFA (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)
- Au:
NSSF STATEMENT (Member Number) (Year)
4. Mfumo wa ‘Member Portal’:
Kupitia Member Portal unaoweza kufikia kwenye tovuti rasmi ya NS-SF (www.nssf.go.tz), utaweza kupata taarifa muhimu kama:
- Taarifa za michango yote iliyowasilishwa na mwajiri wako au michango ya wanachama wa hiari.
- Taarifa za michango (Statements) za mwaka husika.
Jinsi ya Kuingia:
- Ili kutumia Member Portal, hakikisha kwamba umesajili namba yako ya simu na kwamba taarifa zako ziko sahihi. Ikiwa umebadilisha namba yako ya simu au haukuiweka vizuri, tafadhali tembelea ofisi za NSSF ili kuboresha taarifa zako.
Maswali na Majibu:
Kwa maswali zaidi au kupata msaada, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya NS-SF au bofya HAPA.
Kwa hivyo, kupitia programu ya NS-SF Taarifa, WhatsApp, SMS, na Member Portal, unaweza kwa urahisi kufuatilia michango yako na salio lako, ukifanya kazi zako za kifedha kwa urahisi na usalama.
Be the first to comment