Ajira Portal ni jukwaa rasmi linalotolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Tanzania kwa ajili ya kuajiri watumishi wa umma. Kujisajili ni hatua muhimu ili uweze kuomba nafasi za kazi zinazotangazwa. Fuata hatua hizi:
Jinsi ya Kujisajili na Ajira Portal
1: Tembelea Tovuti Rasmi ya Ajira Portal
- Fungua kivinjari (browser) chako na tembelea tovuti ya Ajira Portal kwa kutumia kiungo hiki:
https://portal.ajira.go.tz
2: Bonyeza “Register” au “Jisajili”
- Kwenye ukurasa wa mwanzo wa tovuti, utaona kitufe cha “Register“. Bonyeza hapo ili kufungua fomu ya usajili.
3: Jaza Fomu ya Usajili
- Taarifa za Binafsi: Jaza majina yako kamili, tarehe ya kuzaliwa, namba ya simu, na barua pepe. Hakikisha unatumia barua pepe inayofanya kazi.
- Akaunti ya Kuingia: Tengeneza jina la mtumiaji (username) na nenosiri (password) ambalo utalitumia kuingia.
- Namba ya Kitambulisho: Ingiza NIDA ID au namba ya kitambulisho kingine kinachotambulika.
4: Thibitisha Usajili
- Baada ya kujaza fomu, utapokea barua pepe ya uthibitisho kwenye anwani yako ya barua pepe. Fungua barua pepe hiyo na bonyeza kiungo kilichotumwa ili kuthibitisha akaunti yako.
5: Ingia Kwenye Akaunti
- Rudi kwenye ukurasa wa https://portal.ajira.go.tz na ingia kwa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilounda.
6: Baada ya kuingia:
- Jaza wasifu wako (CV) kwa kujaza taarifa za:
- Elimu yako (shule, chuo, na ngazi ya elimu)
- Uzoefu wa kazi (ikiwa unazo)
- Mafunzo ya ziada au vyeti vingine vinavyohusiana.
- Hakikisha unataarifa zote muhimu kama nakala za vyeti (academic certificates).
7: Angalia Nafasi za kazi
- Tembelea sehemu ya “Jobs” au “Nafasi za Kazi” ili kuona nafasi za kazi zinazotangazwa.
- Soma maelezo ya kazi na uhakikishe unakidhi vigezo kabla ya kuomba.
8: Omba Nafasi ya Kazi
- Bonyeza kitufe cha “Apply Now” kwenye kazi unayotaka kuomba.
- Ambatanisha nyaraka muhimu kama CV, vyeti, na barua ya maombi (application letter).
Vidokezo Muhimu
- Hakikisha taarifa unazojaza ni sahihi na zinaambatana na nyaraka zako.
- Fuata maelekezo yote yaliyotolewa kwenye tangazo la kazi.
- Mara kwa mara tembelea Ajira Portal ili kuona nafasi mpya za kazi.
Ikiwa unakumbana na changamoto, wasiliana na Sekretarieti ya Ajira kupitia mawasiliano yaliyo kwenye tovuti yao.
Be the first to comment