Unakaribishwa katika jukwaa hili maalum lenye makala yenye jina la: Jinsi ya Kujiunga na Vifurushi Vya Startimes 2024 (Kuchagua kifurushi cha startimes). Makala hii imetoa majibu yote ya maswali yako kuhusu kulipa packages za startimes nchini Tanzania.
Kuhusu Jinsi ya Kujiunga na Vifurushi Vya Startimes 2024
StarTimes ni jina la chapa ya Star Media(Tanzania) Limited, ni kampuni ya Teknolojia iliyoanzishwa mwaka 1988 nchini China. StarTimes ni mwanzilishi na mhusika mkuu katika suluhu ya televisheni ya kidijitali nchini China na Afrika, ambapo imepata kuwa na zaidi ya watumiaji milioni 7.
StarTimes inatoa huduma za televisheni za ulimwengu wa kidijitali na satelaiti kwa watumiaji, na hutoa teknolojia kwa nchi na watangazaji ambao wanabadilika kutoka televisheni za analogi hadi za kidijitali. Kufikia Julai 2020, StarTimes ina wasambazaji katika nchi 37, ikihudumia watumiaji milioni 13 wa DVB na watumiaji milioni 20 wa OTT.
Jinsi ya Kulipia Vifurushi vya StarTimes kwa Tigo Pesa
Fatilia hatua hizi jinsi ya kulipia king’amuzi cha startimes kupitia tigo pesa
- Ingiza *150*01# kwenye simu yako kisha piga.
- Chagua “Lipia Bili.”
- Chagua nambari 2 kupata majina ya kampuni.
- Chagua namba 5 “King’amuzi.”
- Chagua namba 2 “StarTimes.”
- Chagua namba 1 “Weka namba ya kumbukumbu.”
- Ingiza namba ya kumbukumbu ambayo ni Smartcard namba ya king’amuzi chako.
- Ingiza kiasi kamili cha kifurushi unachotumia.
- Ingiza namba yako ya siri kuhakiki.
- Utapokea ujumbe kuthibitisha muamala wako wa malipo.
Jinsi ya Kulipia Vifurushi vya StarTimes kwa M-Pesa:
- Ingia kwenye Menu ya M-PESA kwa kupiga *150*00#.
- Chagua namba 4 “Lipia Bili.”
- Chagua “StarTimes” kwenye orodha.
- Ingiza namba ya kumbukumbu ya malipo (Smartcard namba).
- Ingiza kiasi cha pesa unachotaka kulipia.
- Ingiza nambari yako ya siri ya M-Pesa ili kuhakiki muamala.
Jinsi ya Kulipia Vifurushi vya StarTimes kwa Airtel Money:
- Piga *150*60#
- Chagua 5 – Lipia bili
- Chagua 6 – King’amuzi
- Chagua 2 – StarTimes
- Ingiza namba ya smartcard
- Weka kiasi
- Thibitisha kwa kuingiza PIN yako
Je Umefurahia makala hii? toa maoni yako hapa chini, uliza swali lako kwa kutuandikia ujumbe kuhusu Jinsi ya kulipia Vifurushi vya startimes (namna ya kulipa packages za startimes) au mengineyo.
Be the first to comment