Jinsi ya Kukata Tiketi ya Treni Online trc 2024

Jinsi ya Kukata Tiketi ya Treni Online trc 2024

Unakaribishwa katika jukwaa hili maalum lenye makala yenye jina la: Jinsi ya Kukata Tiketi ya Treni Online (www trc co tz online booking online). Makala hii imetoa majibu yote ya maswali yako kuhusu eticketing trc co tz 2024 nchini Tanzania.

Kuhusu Kukata Tiketi ya Treni Online 2024

Shirika la Reli Tanzania (TRC) ni kampuni inayomilikiwa na serikali inayoendesha moja ya mitandao mikuu miwili ya reli nchini Tanzania. Makao Makuu yapo Mchafukoge, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Shirika la Reli na Bandari la Afrika Mashariki lilipovunjwa mwaka 1977 na mali zake kugawanywa kati ya Kenya, Tanzania na Uganda, TRC iliundwa kuchukua shughuli zake nchini Tanzania. Mnamo 1997 kitengo cha meli ya ndani kilikuwa kampuni tofauti.

Jinsi ya Kukata Tiketi ya Treni Online 2024

Fatilia hatua zifuatazo kuhusu Jinsi ya Kukata Tiketi ya Treni Online 2024;

1: Tembelea Tovuti ya Ukataji wa Tiketi ya Treni

Anza safari yako ya kununua tiketi ya treni mtandaoni kwa kutembelea tovuti rasmi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ya mfumo wa mfumo wa kukata tiketi ya Treni https://eticketing.trc.co.tz/.

2: Jaza Taarifa za Safari

Kwenye tovuti, chagua kituo unachotoka na kituo unachokwenda. Bainisha idadi ya wasafiri watakaokuwa kwenye safari hiyo, ikiwemo watoto (wenye umri wa miaka 4-12) au watoto wachanga (wenye umri wa miaka 0-3) watakaosafiri nawe. Baada ya kujaza taarifa hizo, bofya kitufe cha “Fanya Uhifadhi” ili kuendelea.

3: Chagua Treni

Katika hatua hii, utaona orodha ya treni zinazopatikana kwa safari yako iliyochaguliwa. Hakikisha umechagua treni sahihi inayokwenda unakoelekea kwa kubofya kitufe cha “Chagua” kisha uendelee mbele.

4: Chagua Siti

Baada ya kuchagua treni, utaelekezwa kuchagua behewa la daraja unalotaka kusafiria. Chagua siti au kitanda kulingana na idadi ya wasafiri uliowekata awali. Kisha bofya kitufe cha “Endelea Mbele.”

5: Jaza Taarifa za Wasafiri

Katika sehemu hii, jaza taarifa sahihi za wasafiri wote watakaokuwa kwenye safari. Hakikisha unaweka taarifa sahihi za vitambulisho kwa wasafiri wazima. Pia, weka taarifa za mawasiliano ikiwemo namba ya simu au barua pepe ambayo inaweza kutumika kwa urahisi.

6: Thibitisha Taarifa

Kabla ya kuendelea, hakikisha taarifa zote ulizoweka ni sahihi, ikiwemo maelezo ya treni, siti/kitanda, taarifa za wasafiri, na nauli ya safari. Ukishajiridhisha, bofya kitufe cha “Fanya Uhifadhi” ili kukamilisha hatua hii.

7: Fanya Malipo

Mara tu utakapokamilisha uhifadhi, utapokea ujumbe mfupi wa simu (SMS) wenye maelekezo ya jinsi ya kufanya malipo. Unaweza kulipia kwa kutumia simu yako ya mkononi au kwa kutembelea wakala wa TRC.

Je Umefurahia makala hii? toa maoni yako hapa chini, uliza swali lako kwa kutuandikia ujumbe kuhusu www trc co tz online booking online login (Sgr trc online Booking)au mengineyo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*