Jinsi ya Kulipa Kifurushi Cha Azam tv King’amuzi 2024

Jinsi ya Kulipa Kifurushi Cha Azam tv King’amuzi 2024

Unakaribishwa katika jukwaa hili maalum lenye makala yenye jina la: Jinsi ya Kulipa Kifurushi Cha Azam tv King’amuzi 2024 (Jinsi ya Kulipia Azam TV max). Makala hii imetoa majibu yote ya maswali yako kuhusu kulipa King’amuzi cha Azam TV nchini Tanzania.

Kuhusu Jinsi ya Kulipa Kifurushi Cha Azam tv King’amuzi 2024

Azam TV ni huduma ya setilaiti ya Afrika Mashariki ya moja kwa moja inayomilikiwa na Bakhresa Group yenye makao yake jijini Dar es salaam, Tanzania. Ilizinduliwa mwaka wa 2013, huduma hii inatoa huduma za sauti, redio na televisheni kwa waliojisajili, wengi wao wakiwa Tanzania, Malawi, Rwanda, Zimbabwe,Uganda na Kenya.

Mnamo 2021, Azam TV ilipata haki za utangazaji za Ligi Kuu ya Tanzania Bara (Ligi Kuu ya Tanzania) kwa mkataba wa thamani ya Tsh225.6 bilioni. Mkataba huo uliipa haki ya pekee ya daraja la juu kwa miaka 10 ijayo kufuatia ufadhili upya na Shirikisho la Soka Tanzania.

1. Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa M-Pesa

  1. Piga *150*00#
  2. Chagua “Lipa kwa M-Pesa”
  3. Chagua Namba 4 – Malipo Ya Kampuni
  4. Chagua Namba 3 – Chagua Kwenye Orodha
  5. Chagua Namba 1 – King’amuzi
  6. Chagua Namba 5 – Azam Tv – Ok
  7. Ingiza Namba Ya Kumbukumbu: Tz1000xxxx – Ok
  8. Weka Kiasi
  9. Weka Namba Ya Siri
  10. Bonyeza 1 Kuthibitisha

2. Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa Airtel Money:

  1. Piga *150*60#
  2. Chagua Lipa Bili
  3. Chagua chagua biashara
  4. Chagua Vin’gamuzi vya TV
  5. Chagua Azam Pay TV
  6. Weka kiasi
  7. Weka Nambari ya Marejeleo (Nambari ya Akaunti ya Azam TV)
  8. Weka Pini
  9. Bonyeza 1 ili kuthibitisha‚ 2 ili kukataa.

3. Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam kwa Tigo Pesa:

  1. Piga *150*01#
  2. Chagua “Lipa Bili”
  3. Chagua “Pata Namba ya Biashara”
  4. Chagua “5 Kin’gamuzi”
  5. Chagua “Azam Pay Tv”
  6. Fuata hatua kama za M-Pesa

Je Umefurahia makala hii? toa maoni yako hapa chini, uliza swali lako kwa kutuandikia ujumbe kuhusu Jinsi ya Kulipia Azam TV kwa siku (Jinsi ya Kulipia Azam TV kwa Wiki na mwezi) au mengineyo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*