
Unapenda burudani kutoka Azam TV? Kama ni hivyo, huu ni mwongozo bora kabisa kwako. Utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kulipia Azam TV mwaka 2025 kwa njia rahisi, bila kwenda kwa wakala wala kusumbuka.
Sasa unaweza kufurahia mechi za Ligi Kuu Tanzania, tamthilia kali, habari moto, na vipindi vya elimu ukiwa nyumbani tu. Na cha kufurahisha zaidi? Malipo yanawezekana kupitia simu yako ya mkononi!
Kwa Nini Uichague Azam TV?
Azam TV imekuwa chaguo pendwa kwa Watanzania kwa sababu ya:
- Vifurushi vya bei nafuu
- Mchanganyiko wa burudani, michezo, elimu na habari
- Chaneli zinazofaa familia nzima
Lakini kabla hujaanza kuangalia muvi au mechi, ni lazima kwanza kulipia kifurushi cha Azam TV.
Orodha ya Vifurushi vya Azam TV 2025
Chagua kifurushi kinachokufaa kulingana na bajeti yako:
- Azam Lite – TZS 8,000
Burudani ya msingi kwa gharama nafuu - Azam Pure – TZS 13,000
Chaneli zaidi kwa ladha zaidi - Azam Plus – TZS 20,000
Uhondo wa kati kwa familia nzima - Azam Play – TZS 35,000
Burudani ya kiwango cha juu, bila kukosa chochote
Pia kuna DTT Packages kama Saadani, Mikumi, Ngorongoro, na Serengeti – zote kwa bei sawa na vifurushi vya kawaida.
Jinsi ya Kulipia Azam TV kwa Urahisi
Jinsi ya Kulipia Azam TV kwa Simu Mwaka 2025
Leo hii, huitaji kutoka nje kutafuta sehemu ya kulipia. Tumia tu simu yako kupitia huduma ya M-Pesa, Airtel Money au Tigo Pesa.
✅ 1. Kulipia Azam TV kwa M-Pesa
- Piga
*150*00#
- Chagua Lipa kwa M-Pesa
- Chagua Malipo ya Kampuni (Namba 4)
- Chagua Chagua kwenye Orodha (Namba 3)
- Chagua King’amuzi (Namba 1)
- Chagua Azam TV (Namba 5)
- Ingiza Namba ya kumbukumbu (mfano: Tz1000xxxx)
- Weka kiasi cha kulipia
- Ingiza namba ya siri
- Bonyeza 1 kuthibitisha
✅ 2. Kulipia Azam TV kwa Airtel Money
- Piga
*150*60#
- Chagua Lipa Bili
- Chagua Biashara
- Chagua Vin’gamuzi vya TV
- Chagua Azam Pay TV
- Ingiza kiasi cha kulipia
- Ingiza namba ya marejeleo (account number ya Azam TV)
- Ingiza Pini yako
- Bonyeza 1 kuthibitisha
✅ 3. Kulipia Azam TV kwa Tigo Pesa
- Piga
*150*01#
- Chagua Lipa Bili
- Chagua Pata Namba ya Biashara
- Chagua King’amuzi (Namba 5)
- Chagua Azam Pay TV
- Fuata maelekezo kama ilivyo kwa M-Pesa
Hitimisho: Furahia Burudani Bila Kukatizwa
Sasa unajua jinsi ya kulipia Azam TV kwa urahisi mwaka 2025. Huna haja ya kusumbuka tena na foleni au kutafuta wakala. Tumia simu yako, lipia kifurushi, na burudika bila bugudha!
Be the first to comment