
Kama unapenda soka, basi unajua raha yake ni kubwa zaidi pale unaposhuhudia timu yako ukipiga kelele jukwaani, siyo tu kwenye runinga. Lakini ili kufika uwanjani, jambo la kwanza ni kununua tik-eti ya mpira. Na sasa mambo yamekuwa rahisi zaidi — unaweza kununua tiketi za mpira kwa Airtel Money bila kusumbuka, popote ulipo!
Hapa chini tumeandaa mwongozo mwepesi, hatua kwa hatua, utakusaidia kununua tiketi zako haraka na salama kwa kutumia simu yako ya mkononi.
Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Airtel Money
- Piga 15060#
Anza kwa kupiga 15060# kwenye simu yako. - Chagua 5 – Lipa Bili
Katika menyu ya Airtel Money, bonyeza 5 kuchagua “Lipa Bili”. - Chagua # – Next
Hii itakupeleka kwenye chaguo zaidi. - Chagua 8 – Malipo Mtandao
Bonyeza 8 ili kuingia kwenye sehemu ya kulipa kupitia mtandao. - Chagua 1 – Tiket za Michezo
Hapa ndipo unapata nafasi ya kuchagua mechi unayotaka. - Chagua 1 – Football Tickets
Kwa mashabiki wa soka, chagua chaguo hili. - Chagua Mechi Unayotaka
Tafuta mechi yako pendwa kwenye orodha inayotolewa. - Chagua Aina ya Tiketi
Iwe ni VIP, kawaida au jukwaa lolote – chagua unalolitaka. - Weka Namba ya N-Card
Hii ni kwa ajili ya kuthibitisha tiketi yako. - Ingiza Namba ya Siri ya Airtel Money
Hakikisha unaingiza PIN yako kwa usahihi. - Thibitisha Malipo
Ukimaliza, utapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo yako na tiketi imekatwa rasmi!
Mapendekezo: Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira kwa Vodacom M-Pesa (Mwongozo Rahisi)

Kwa Nini Utumie Airtel Money Kununua Tiketi za Mpira?
- Ni Rahisi na Haraka – Hakuna foleni, hakuna safari hadi kwenye ofisi za tik-eti.
- Salama Zaidi – Hutabeba pesa taslimu, kila kitu kiko kwenye simu yako.
- Unapatikana Wakati Wowote – Iwe ni usiku au mchana, unaweza kununua tike-ti yako.
- Huduma Bora kwa Wateja – Ukikwama, timu ya msaada iko tayari kukusaidia.
Ushauri wa Haraka
Kabla hujanunua, hakikisha una salio la kutosha kwenye akaunti yako ya Airtel Money na pia umeweka namba yako ya N-Card sahihi.
Tazama Mechi Uipendayo Bila Stress!
Sasa unajua jinsi ya kununua tike-ti ya mpira kwa Airtel Money. Usikose mechi kwa sababu ya tike-ti — fuata tu hatua hizi rahisi na ufurahie burudani ukiwa uwanjani!
Be the first to comment