Jinsi ya Kupata Leseni Online kupitia Mfumo wa TAUSI unatoa njia rahisi kwa watumiaji kujiandikisha na kuomba leseni za biashara mtandaoni. Ili kuhakikisha unafanikiwa, fuata maelekezo yafuatayo.
NJIA KUU MBILI ZA KUJISAJILI
Mfumo wa TAUSI unatoa njia mbili za kujisajili. Chagua mojawapo kulingana na urahisi wako:
1. Kujisajili kwa Kujibu Maswali ya NIDA
Njia hii inahitaji ujibu maswali yanayohusu taarifa zako za NIDA kwa usahihi.
Hatua za Kufanya:
- Chagua chaguo la kwanza kwenye ukurasa wa usajili.
- Ingiza namba yako ya NIDA kwenye kisanduku husika kisha bofya Search.
- Jibu maswali yote kuhusu taarifa zako za NIDA kwa usahihi.
- Mfumo utakupokea ukifanikiwa kujibu maswali.
- Bonyeza kitufe cha Continue kuendelea.
KUMBUKA:
- Hakikisha maswali yote yanajibiwa kwa ufasaha ili mfumo uruhusu usajili wako.
2. Kujisajili kwa Kutumia Nywila Mahususi (OTP)
Hii ni njia nyingine inayotumia ujumbe wa nywila mahususi unaotumwa kwa simu yako.
Hatua za Kufanya:
- Chagua chaguo la pili kwenye ukurasa wa usajili.
- Ingiza namba yako ya NIDA na namba ya simu iliyosajiliwa na NIDA.
- Bonyeza Request OTP.
- Subiri ujumbe wa maandishi (SMS) kutoka namba 15200 yenye namba sita (OTP).
- Ingiza OTP kwenye mfumo na jaza barua pepe yako, namba ya simu, na tengeneza nywila.
KUINGIA KATIKA MFUMO WA TAUSI
Baada ya kujisajili, unaweza kufuata hatua hizi kuingia:
- Unganisha kifaa chako na intaneti.
- Fungua kivinjari (browser) na andika anuani https://tausi.tamisemi.go.tz.
- Bonyeza Sign In na uingize taarifa zako za kuingia.
KUINGIZA TAARIFA ZA TIN KWENYE MFUMO
Kama unahitaji kuongeza taarifa za TIN (Tax Identification Number):
- Bonyeza alama za nukta tatu upande wa juu kulia kisha chagua My Profile.
- Bonyeza INDIVIDUAL TIN DETAILS kisha Update Now.
- Soma masharti na hakikisha unakubaliana nayo.
- Ingiza namba yako ya TIN na bonyeza Search.
KUMBUKA:
- Ikiwa biashara ni ya kampuni, kampuni itahitaji kuwasilisha barua ya kumtambulisha mwakilishi wake.
Jinsi ya Kupata Leseni Online
- Fungua menyu kuu kwa kubonyeza alama ya mistari minne na chagua Application.
- Chagua Business License na bonyeza Apply Now.
- Jaza mkoa, halmashauri, na maelezo mengine ya biashara kama ifuatavyo:
- Jina la biashara
- Kundi kuu la biashara
- Aina ya biashara
- Muda wa leseni
- TAX CLEARANCE number
- Chagua eneo la biashara, kata, mtaa, block, na plot number.
- Pakia viambatanisho vinavyohitajika (vyawe PDF na visizidi 2 MB).
Baada ya kukamilisha, hakikisha taarifa zote ni sahihi na bonyeza Save ili kutuma maombi yako.
UPAKUAJI WA LESENI YA BIASHARA
- Baada ya maombi yako kupitishwa, utapokea Control Number kwa ajili ya malipo.
- Lipa malipo yanayohitajika na uchapishe leseni yako.
- Bonyeza Download kupakua leseni.
Kwa kufuata maelekezo haya, utaweza kutumia mfumo wa TAUSI kwa ufanisi na haraka!
Be the first to comment