Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu kwa Haraka 2024

Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu kwa Haraka 2024

Unakaribishwa katika jukwaa hili maalum lenye makala yenye jina la: Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu kwa Haraka 2024 (jinsi ya kupata namba ya nida kwa haraka). Makala hii imetoa majibu yote ya maswali yako kuhusu Kuangalia usajili wa line nchini Tanzania.

Kuhusu Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu 2024

National Identification Authority (NIDA) /Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni chombo cha kusimamia Vitambulisho vya Taifa nchini Tanzania.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ina jukumu la usajili na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na Kisheria. Wakazi halali wanastahiki kadi ya NIDA ikiwa wana kibali halali cha mkazi na pasipoti halali isiyopungua miezi sita.

Wazo la kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilizaliwa mwaka 1968 katika kikao cha “Interstate Intelligence Gathering” kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia.

Kwa wakati huo nchi za Kenya na Zambia tayari zilikuwa na Vitambulisho vyao vya Taifa. Iliazimiwa kwamba ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne ni lazima nchi za Uganda na Tanzania nazo zikatoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wao.

Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2024

Kupata namba ya NIDA kumekuwa rahisi zaidi kuliko hapo awali. Sasa mtu yeyote anaweza kupata namba ya NIDA kwa urahisi na haraka kupitia simu ya mkononi, bila kujali mahali alipo au aina ya simu anayotumia. Hadi hivi sasa kuna njia kuu mbili za kupata namba ya NIDA kwa kutumia simu ya mkononi. Njia hizi ni kama zifuatazo;

  • Kupitia USSD
  • Kupitia SMS

Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia USSSD

USSD (Unstructured Supplementary Service Data) ni njia rahisi na ya haraka ya kupata namba ya NIDA bila kuhitaji muunganisho wa intaneti. Fuata hatua hizi rahisi:

  1. Piga *152*00# kwenye simu yako ya mkononi.
  2. Chagua namba 3 (Ajira na Utambuzi).
  3. Chagua namba 2 (NIDA).
  4. Ingiza majina yako matatu (3) uliyojisajili (Mfano: Dan John Sele).
  5. Ingiza namba ya simu uliyojaza kwenye fomu ya maombi (Mfano: 0XXXXXXX).
  6. Kubali ombi lako.
  7. Utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye namba yako ya NIDA.

Huduma hii kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa Airtel na Vodacom.

Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia SMS

Njia nyingine rahisi ya kupata namba yako ya NIDA ni kupitia SMS. Fuata hatua hizi:

  1. Andika ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye majina yako matatu (3) uliyojisajili (Mfano: Dan John Sele).
  2. Tuma SMS hiyo kwenda namba 15096.
  3. Utapokea ujumbe wa kujibu wenye namba yako ya NIDA. Huduma hii ni bure na inapatikana kwa mitandao yoteya simu nchini Tanzania.

Huduma hii inapatikana kwa watumiaji wa mitandao ya simu ya Airtel na Vodacom.

Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka Mtandaoni

Kuangalia namba ya NIDA mtandaoni ni njia rahisi na ya haraka ya kuhakikisha unapata namba yako bila kuhitaji kwenda ofisi za NIDA. Pia, inakupa uhakika wa kuwa na namba yako popote ulipo, kwa kutumia tu kifaa chako cha kielektroniki kama simu au kompyuta.

Ili kukagua namba yako ya NIDA mtandaoni, unahitaji kuwa na taarifa zifuatazo:

  1. Jina Kamili: Hakikisha unajua jina lako la kwanza na la mwisho kama lilivyo kwenye nyaraka zako za usajili.
  2. Tarehe ya Kuzaliwa: Tumia muundo wa tarehe (DD-MM-YYYY).
  3. Majina ya Mama: Ingiza jina la kwanza na la mwisho la mama yako kama lilivyoandikwa kwenye nyaraka zako za usajili.
  4. Muunganisho wa Mtandao: Unahitaji kuwa na muunganisho thabiti wa intaneti ili kufanikisha mchakato huu.

Je Umefurahia makala hii? toa maoni yako hapa chini, uliza swali lako kwa kutuandikia ujumbe kuhusu vitambulisho nida go tz (www nida go tz) au mengineyo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*