Unakaribishwa katika jukwaa hili maalum lenye makala yenye jina la: Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS 2024 (jinsi ya kupata namba ya nida kwa haraka). Makala hii imetoa majibu yote ya maswali yako kuhusu Kupata namba ya nida kupitia sms nchini Tanzania.
Kuhusu Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS 2024
National Identification Authority (NIDA) /Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni chombo cha kusimamia Vitambulisho vya Taifa nchini Tanzania.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ina jukumu la usajili na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na Kisheria. Wakazi halali wanastahiki kadi ya NIDA ikiwa wana kibali halali cha mkazi na pasipoti halali isiyopungua miezi sita.
Wazo la kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilizaliwa mwaka 1968 katika kikao cha “Interstate Intelligence Gathering” kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia.
Kwa wakati huo nchi za Kenya na Zambia tayari zilikuwa na Vitambulisho vyao vya Taifa. Iliazimiwa kwamba ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne ni lazima nchi za Uganda na Tanzania nazo zikatoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wao
Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS 2024
Fatilia Hatua Hizi ili kuweza Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS. Njia hii itakusaidia Jinsi Ya Kuangalia Namba Ya NIDA Airtel, Namba ya NIDA kwa tigo,Jinsi ya Kuangalia Namba ya NIDA Vodacom
1. Fungua Sehemu ujumbe mpya.
Hakikisha una salio la kutosha kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenye simu yako.
2. Andika ujumbe mfupi
Fuata muundo huu unapoandika ujumbe mfupi : jina la kwanza *jina la mwisho* tarehe ya kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama. Kwa Mfano: Mujuni*Kukushaba*12031993*Anna*Guta
3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15096.
Huduma hii ni bure kabisa, hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu gharama.
4. Subiri ujumbe wa kujibu kutoka NIDA.
Ujumbe huu utakuwa na namba yako ya NIDA. Hakikisha unahifadhi namba hii mahali salama kwani utahitaji kuitumia mara kwa mara.
Je Umefurahia makala hii? toa maoni yako hapa chini, uliza swali lako kwa kutuandikia ujumbe kuhusu Namba ya nida kwa sms 15096 au mengineyo.
Nimefurahi sana