Jeshi la Polisi Tanzania kwa sasa linatoa huduma ya Loss Report kupitia njia ya mtandao badala ya vituo vya polisi. Huduma hii ni rahisi na ya haraka kwa gharama ya TZS 1,000 tu.
JINSI ya Kupata Polisi Loss Report Online
Fuata hatua hizi:
1. Fungua Tovuti Rasmi ya Loss Report
Tembelea tovuti ya Jeshi la Polisi kupitia hii link.
2. Chagua Aina ya Usajili
- Kama wewe ni mteja mpya, bofya “Sajili Mali Iliyopotea”.
- Kama umeshajisajili, bofya “Mtumiaji Aliyesajiliwa” ili kuendelea.
3. Jaza Taarifa Zako Binafsi
Unapofungua akaunti, utahitajika kujaza taarifa zifuatazo:
- Utaifa
- Majina yako kamili
- Jinsia
- Aina ya Kitambulisho (mfano: NIDA)
- Namba ya Kitambulisho
- Picha ya Pasipoti Sizi yenye ukubwa wa width 480px na height 640px
4. Jaza Maelezo ya Mali Iliyopotea
Ingiza maelezo sahihi ya kitu kilichopotea, kama vile jina, tarehe, na mahali upotevu ulipotokea.
5. Lipia TZS 1,000 Kupitia GePG
Baada ya kujaza taarifa, utapokea namba ya udhibiti kama ifuatayo: 99XXXXXXXX.
- Lipa shilingi 1,000 kupitia simu yako ya mkononi au benki inayotumia mfumo wa malipo wa Serikali (GePG).
6. Pakua Loss Report Yako
Baada ya malipo, unaweza kupakua Loss Report yako moja kwa moja kutoka tovuti.
Vidokezo Muhimu
- Ripoti ya Loss Report si uchunguzi wa polisi, bali ni nyaraka ya kuripoti upotevu wa mali.
- Kuripoti taarifa za uongo ni kosa la jinai linaloadhibiwa kisheria.
Linki Muhimu za Haraka
Maelezo Zaidi Kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania
Jeshi la Polisi Tanzania ni chombo cha kitaifa kinachosimamia:
- Sheria na utaratibu
- Ulinzi wa maisha na mali
- Kuzuia, kugundua, na kuchunguza uhalifu
Idara kuu za Jeshi la Polisi ni:
- Utawala na Usimamizi wa Rasilimali
- Uendeshaji
- Uchunguzi wa Jinai
- Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam
- Polisi Zanzibar
Kwa maelezo zaidi au msaada, wasiliana na Jeshi la Polisi Tanzania kupitia:
Barua pepe: [email protected]
Be the first to comment