
Mechi kati ya Simba SC na JKT Tanzania itapigwa leo, Jumatatu tarehe 5 Mei 2025, katika mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Mashabiki wanatarajia pambano lenye ushindani mkubwa kutokana na historia ya timu hizi.
Muda na Mahali pa Mechi
- Tarehe: Jumatatu, 5 Mei 2025
- Muda: Saa 10:00 jioni
- Uwanja: Meja Jenerali Isamuyo.
Simba na Jkt Walipokutana
Tangu mwaka 2019, Simba SC na JKT Tanzania wamekutana mara 9 katika mashindano rasmi. Katika mikutano hiyo:
- Simba SC: imeshinda mechi 8
- JKT Tanzania: imeshinda mechi 1
- Sare: hakuna
- Jumla ya mabao: Simba SC imefunga mabao 17, JKT Tanzania mabao 2
Mechi ya mwisho kati ya timu hizi ilichezwa tarehe 24 Desemba 2024, ambapo Simba SC iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania.
Kikosi cha Simba vs Jkt Tanzania leo
Simba SC (Kocha: Fadru Davis):
- Kipa: Moussa Cammara
- Mabeki: Shomary Kapombe, Mohamed Hussein, Abdurazack Hamza, Che Malone
- Viungo: Elie Mpanzu, Yusuph Kagoma, Charles Ahoua, Denis Kibu, Fabrice Ngoma
- Mshambuliaji: Lionel Ateba
Wachezaji wa Akiba:
- Ally Salim
- Valentine Nouma
- David Kameta ‘Duchu’
- Desse Mukwala
- Hussein Kazi
- Edwin Balua
- Mzamiru Yassin
JKT Tanzania FC (Kocha: Hamad Ally):
- Kipa: Jakoub Seleman
- Mabeki: Martin Kigi, Davd Brayson, Wema Sadock, Edson Katanga
- Viungo: Hassan Dilunga, Najimu Magulu, Saidi Ndemla
- Washambuliaji: Sixtus Sabilo, John Bocco , Shiza Ramadhani
Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Simba SC ikilenga kuendeleza rekodi yake nzuri dhidi ya JKT Tanzania, na JKT Tanzania ikisaka ushindi muhimu dhidi ya wapinzani wao wa muda mrefu.
Angalia Hapa: Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025
Be the first to comment