Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo 08/03/2024

Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo 08/03/2024

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo watashuka dimbani kuwakabili mahasimu wao wa jadi, Yanga SC, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchuano huu utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ukianza majira ya saa 1:30 usiku, na umevuta hisia kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka nchini kutokana na upinzani mkali wa timu hizi kongwe.

Kariakoo Dabi: Mechi ya Heshima na Ubabe

Kariakoo Dabi ni miongoni mwa mechi zinazovutia hisia kubwa kila msimu, huku mashabiki wa pande zote mbili wakitarajia ushindi. Simba SC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi msimu huu wa 2024/25. Kocha wao, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa wamejiandaa kikamilifu kupambana na Yanga SC kwa lengo la kupata alama tatu muhimu.

Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesisitiza kuwa timu yake imejiandaa kwa mbinu kabambe, akitamba na mkakati wa “Tripple Frontier”. “Tutawapiga mapigo matatu makubwa; kwanza pumzi ya moto, pili tutawaangamiza, na mwisho tutamalizia na ubaya ubwela,” alisema Ally, akionyesha ari kubwa ya kupata ushindi katika mchezo wa leo.

Simba SC: Dhamira ya Kudumisha Rekodi

Simba wanatarajia kutumia mchezo huu kuimarisha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi na kuendeleza rekodi yao nzuri msimu huu. Katika michezo yao mitano ya hivi karibuni, wameshinda mara nne na kutoka sare mara moja. Hata hivyo, wanakabiliwa na changamoto ya majeruhi ambapo wachezaji kama Ayoub Lakred na Aishi Manula bado hawajawa fiti kikamilifu.

Utabiri wa Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo

Kocha Fadlu Davids anatarajiwa kutangaza rasmi kikosi chake muda mfupi kabla ya mechi, lakini kutokana na viwango vya wachezaji katika michezo iliyopita, kikosi kinachotarajiwa kinaweza kuwa:

  • Kipa: Camara
  • Beki wa Kulia: Shomari Kapombe
  • Beki wa Kushoto: Mohammed Hussein
  • Mabeki wa Kati: Abdlazack Hamza, Che Malone
  • Kiungo Mkabaji: Yusuph Kagoma
  • Winga wa Kulia: Kibu Denis
  • Kiungo wa Katikati: Debora Fernandes
  • Winga wa Kushoto: Ellie Mpanzu
  • Kiungo Mshambuliaji: Jean Ahoua
  • Straika: Leonel Ateba

Changamoto na Matarajio

Simba SC wana azma ya kudumisha kasi yao ya ushindi licha ya changamoto ya majeruhi. Mashabiki wanatarajia mchezo wenye ushindani mkali, huku Simba wakitafuta ushindi ili kupunguza pengo la alama dhidi ya vinara wa ligi, Yanga SC. Kwa upande wa Yanga, nao wanatarajia kuimarisha uongozi wao kwa kupata ushindi dhidi ya wapinzani wao wa jadi.

Je, Simba wataendeleza rekodi yao ya kutopoteza, au Yanga watawatungua na kuendeleza ubabe wao kwenye ligi? Jibu litapatikana baada ya dakika 90 za mchezo mkali kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa!

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*