
Unataka kubadilisha faili la Word kuwa PDF bila kupakua app yoyote? Upo mahali sahihi! Njia hii ni rahisi sana na hufanya kazi kwa haraka, mradi tu una intaneti kwenye simu au kompyuta yako.
Twende moja kwa moja kwenye hatua:
Hatua ya Kwanza:
Tembelea tovuti hii ambayo ni ya Watanzania na inafanya kazi vizuri kuliko nyingi nilizowahi kutumia. Bonyeza hapa 👉 Tembelea Tovuti Hapa

Kumbuka: Hakikisha kifaa chako kimeunganishwa na intaneti.
Hatua ya Pili: Chagua na Pakia Faili la Word
Ukifika kwenye tovuti:
- Bofya sehemu iliyoandikwa “Choose File” au dondosha faili lako kwenye eneo la bluu.
- Chagua faili la Word (.docx) kutoka kwenye simu au kompyuta yako.

Kidokezo: Hakikisha faili unalotaka kubadilisha ni la aina ya .docx
.
Hatua ya Tatu: Bofya “Convert to PDF”
Baada ya kupakia faili:
- Litajitokeza kwenye sehemu ya maandalizi.
- Bofya kitufe cha “Convert to PDF.”
- Subiri kwa muda mfupi, usifunge ukurasa hadi mchakato umalizike.

Unaweza pia kuongeza zaidi ya faili moja kwa kubofya alama ya jumlisha (+) upande wa juu kushoto.
Hatua ya Mwisho: Pakua Faili Lako la PDF
Baada ya mchakato kukamilika:
- Utaona ujumbe wa mafanikio.
- Bofya sehemu ya “Download” kupakua faili lako la PDF.
Rahisi hivyo tu! Hakuna app, hakuna usumbufu, hakuna malipo!
Manufaa ya Njia Hii
- Huhitaji kupakua app yoyote.
- Ni bure kabisa.
- Unaweza kutumia mara nyingi unavyotaka.
- Inafanya kazi kwenye simu au kompyuta.
Unataka Kujua Zaidi?
Tumia njia hii sasa kubadilisha Word kuwa PDF bila kutumia app yoyote! Kama ulikuwa unahangaika kutafuta njia, basi umeipata sahihi kabisa.
Be the first to comment