
Majina walioitwa kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025, Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza orodha ya waombaji walioitwa kwenye usaili wa ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Jumla ya waombaji 33,990 wamechaguliwa kushiriki kwenye mchakato wa usaili huu muhimu.
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 25 Aprili hadi 11 Mei 2025 katika mikoa mbalimbali nchini. Waombaji wanatakiwa kufika kwenye vituo walivyopangiwa kwa tarehe na muda uliopangwa, wakiwa na nyaraka muhimu zilizoorodheshwa kwenye tangazo rasmi.
Nyaraka Muhimu Kufika Nazo Katika Usaili:
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA
- Vyeti halisi vya elimu (cheti cha kidato cha nne/sita na vyeti vya taaluma)
- Cheti cha kuzaliwa
- Picha ndogo za pasipoti (passport size) 2
- Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa/kijiji
Maelekezo Muhimu:
- Hakikisha unafika kwenye kituo cha usaili kwa muda uliopangwa.
- Kuchelewa au kutokufika kutachukuliwa kama umejiondoa katika mchakato.
- Jeshi la Polisi halihusiki na mtu yeyote anayetoa ahadi ya ajira kwa njia zisizo rasmi — epuka matapeli.
Angalia Majina walioitwa kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025 Hapa:
Kumbuka: Hakikisha umeangalia jina lako vizuri na kituo cha usaili ulichopangiwa. Endelea kufuatilia tovuti rasmi ya Jeshi la TZPolisi au mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi.
Be the first to comment