
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika awamu ya pili kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Orodha hiyo inajumuisha majina ya waliopata nafasi kwenye kozi mbalimbali za shahada ya kwanza, diploma na programu nyingine. Kama uliomba kujiunga UDOM, sasa unaweza kuangalia kama jina lako limo kwenye orodha ya waliochaguliwa.
✅ Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa UDOM 2024/2025
Kuna njia rahisi tatu za kuangalia kama umechaguliwa kujiunga UDOM:
1. Kupitia Ujumbe wa Simu (SMS)
Kama umechaguliwa, utapokea ujumbe mfupi kwenye simu uliyoitumia wakati wa kutuma maombi. Ujumbe huo utaonesha kozi uliyochaguliwa.
2. Kupitia Mfumo wa Udahili wa UDOM (UDOM OAS)
Tembelea tovuti: https://application.udom.ac.tz
Kisha fuata hatua hizi:
- Ingia kwa jina la mtumiaji (username) na nenosiri ulilotumia wakati wa kuomba.
- Ukishaingia, utaona taarifa kama umechaguliwa.
- Thibitisha kwa kutumia namba ya uthibitisho (special code) utakayopokea kwa SMS.
3. Kupitia PDF za Majina ya Waliochaguliwa
UDOM pia imetoa orodha ya majina kupitia dokumenti za PDF. Hizi zinapatikana mtandaoni na zinajumuisha:
- Waliochaguliwa kozi moja
- Waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja
- Waliochaguliwa diploma
Waliochaguliwa Zaidi ya Chuo Kimoja – Thibitisha Mapema
Kama umechaguliwa zaidi ya chuo kimoja, unapaswa kuthibitisha chuo kimoja tu kati ya tarehe 5 hadi 21 Oktoba 2024. Tumia namba ya uthibitisho utakayopokea kwa SMS au barua pepe.
Ukikosa namba hiyo, tembelea mfumo wa chuo husika au tovuti ya TCU: www.tcu.go.tz
Majina ya Waliochaguliwa UDOM Awamu ya Pili 2025/2026
Kama hukuchaguliwa awamu ya kwanza wala ya pili, bado una nafasi!
Awamu ya tatu ya udahili itafanyika kuanzia 5 hadi 9 Oktoba 2024. Hii ni fursa ya mwisho kwa mwaka huu, usikose!
Kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Chuo Kikuu cha Dodoma kilianzishwa mwaka 2007, na ni moja ya vyuo vikuu vikubwa zaidi Tanzania. Kiko takribani kilomita 7 mashariki mwa jiji la Dodoma, na kina uwezo wa kudahili hadi wanafunzi 40,000.
UDOM kina vyuo 6, shule 3, na taasisi 2 – zote zikiwa na miundombinu na huduma bora kwa ajili ya wanafunzi na walimu.
Chuo hiki ni fahari ya taifa kwa sababu kimejengwa kwa fedha za ndani, kikilenga kusaidia maendeleo ya nchi na kutoa elimu bora kwa vijana wa Kitanzania.
Angalia Hapa: Majina ya Waliopata Mkopo 2025/2026 HESLB
Be the first to comment