
Majina ya Walioitwa Kazini UTUMISHI, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni taasisi ya serikali inayosimamia ajira na uchaguzi wa wafanyakazi wa nafasi mbalimbali ndani ya sekta ya umma. Kuitwa kazini kwa mwezi Aprili 2025 ni fursa nzuri kwa watu wanaotafuta ajira katika taasisi mbalimbali za serikali nchini Tanzania.
PSRS ni idara ya serikali iliyo huru, iliyoanzishwa rasmi kwa ajili ya kurahisisha mchakato wa kuajiri wafanyakazi katika utumishi wa umma. Sekretarieti hii iliundwa chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 na kufanyiwa marekebisho kupitia Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1).
Kuitwa Kazini UTUMISHI ni Nini?
“Kuitwa Kazini UTUMISHI ni tangazo rasmi kutoka kwa PSRS kuhusu watu waliopatikana kufaa kwa nafasi mbalimbali za ajira katika taasisi za serikali. Nafasi hizi zipo katika sekta kama afya, elimu, ustawi wa jamii na nyinginezo. Mchakato wa kuajiri unahusisha hatua mbalimbali kama vile kuomba kazi, kuchambua maombi, kufanya tathmini na kuchagua waliokidhi vigezo.
Jinsi ya Kuangalia Kama Umeitwa Kazini:
Ili kujua kama umeitwa kazini kupitia UTUMISHI, tembelea tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira (PSRS). Wameweka orodha ya majina ya waliochaguliwa, hivyo hakikisha unaangalia jina lako kwenye orodha hiyo. Pia, orodha hiyo imeshatolewa hapa chini kwa urahisi zaidi.
Orodha ya Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi – Aprili 2025
Hii hapa ni orodha ya waliopangiwa ajira kupitia tangazo la ajira la mwezi Aprili, 2025. Watu hawa walituma maombi ya kazi na sasa wamechaguliwa kwa ajira ya kudumu katika taasisi mbalimbali za serikali.
Matangazo ya Kuitwa Kazini yaliyotolewa mwezi Aprili 2025 ni pamoja na:
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI – Benki Kuu ya Tanzania (BOT) – 17/04/2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI – Taasisi Mbalimbali za Umma – 17/04/2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI – Taasisi Mbalimbali za Umma – 09/04/2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI – Walimu na Kada Mbalimbali – 02/04/2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) – 02/04/2025
Angalia Hapa: Jinsi ya Kujisajili na Ajira Portal
Be the first to comment