
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza majina ya waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
TAREHE NA MAHALI PA KURIPOTI
Wahusika wote wanatakiwa kufika katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 18 Mei, 2025 bila kukosa.
Mtu yeyote ambaye hataripoti ndani ya muda uliopangwa hatapokelewa na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.
JINSI YA KUFIKA CHUONI
Shuka kituo cha Kabuku, ambacho kiko kilomita 12 kutoka chuoni. Chuo kimeandaa utaratibu maalumu wa kuwapokea waliochaguliwa kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku katika siku zilizotajwa hapo juu.
GHARAMA BINAFSI
Mhusika atapaswa kujigharamia:
- Nauli ya kwenda chuoni
- Chakula na malazi kwa kipindi chote kabla ya kupokelewa rasmi chuoni
VYETI NA NYARAKA MUHIMU
Kila mhusika anatakiwa kuja akiwa na:
- Vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi alioomba
- Cheti cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA
- Leseni hai kwa walioomba nafasi ya udereva
Kila cheti kiambatane na nakala tatu (3).
Angalizo: Mtu yeyote ambaye majina yake yatatofautiana kati ya vyeti vya shule/taaluma, cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha NIDA, hatapokelewa chuoni.
UPIMAJI WA AFYA
Wahusika wote watafanyiwa vipimo vya:
- Afya ya mwili
- Afya ya akili
- Kipimo cha ujauzito kwa wanawake
Mtu yeyote atakayebainika kuwa na kasoro za kiafya hataruhusiwa kuendelea na mafunzo na atarudishwa nyumbani kwa gharama zake.
VIFAA VYA KUJA NAVYO
Wahusika wote wanatakiwa kuja na:
- Mashuka mawili (rangi ya bluu)
- Mto mmoja na foronya mbili (rangi ya bluu)
- Chandarua (cha duara, rangi ya bluu)
- Ndoo ya plastiki ya lita 20
- Sahani na kikombe cha bati
- Fedha kwa matumizi binafsi
- Kadi ya bima ya afya kwa walionazo
VIFAA VITAKAVYONUNULIWA CHUONI
Wahusika watanunua kwenye duka la chuo:
- Raba za michezo
- Fulana (T-shirt) ya rangi ya bluu
- Madaftari makubwa (counter books 4 quire – 5 pcs)
- Vifaa vya michezo (track suit, bukta bluu, na fulana)
- Kalamu
Be the first to comment