
Majina ya Waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Pili, Je, umeomba mkopo wa elimu ya juu kupitia HESLB kwa mwaka wa masomo 2025/2026? Kama ndio, basi huu ni wakati wa kuangalia majibu yako! Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza awamu ya pili ya wanafunzi waliopata mikopo kwa ngazi mbalimbali—kuanzia diploma hadi shahada ya uzamivu.
Wanafunzi 30,311 wa Shahada ya Kwanza Wapewa Mikopo
Katika tangazo hili la pili, wanafunzi 30,311 wa shahada ya kwanza wamefanikiwa kupata mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 93.7. Hii inafanya idadi ya wanafunzi wote waliopata mikopo kwa awamu ya kwanza na pili kufikia 51,645, na jumla ya mikopo kufikia shilingi bilioni 163.8.
Kati yao, 43% ni wanawake na 57% ni wanaume.
Diploma, Uzamili na Uzamivu Pia Wanufaika
- Wanafunzi wa Diploma: 2,157 wamepata mikopo ya takribani TSh bilioni 5.6
- Wanafunzi wa Uzamili (Masters): 45 wamepata mikopo ya TSh milioni 205.6
- Wanafunzi wa Uzamivu (PhD): 16 wamepata mikopo ya TSh milioni 215.6
Awamu ya Tatu Inakuja Hivi Karibuni
HESLB bado inapokea taarifa za udahili kutoka vyuo mbalimbali. Awamu ya tatu ya mikopo inatarajiwa kutangazwa ndani ya siku chache. Endelea kufuatilia!
Samia Scholarship Yawanufaisha Wanafunzi 588
Wanafunzi 588 wa shahada ya kwanza wamepata ufadhili wa ‘Samia Scholarship’ kwa mwaka huu. Ufadhili huu unathaminiwa kwa zaidi ya TSh bilioni 2.9, na unalenga wanafunzi waliofanya vizuri katika sayansi, teknolojia, uhandisi, hisabati, na tiba.
Jinsi ya Kuangalia Kama Umepata Mkopo wa HESLB 2025/2026
Unaweza kuangalia kwa urahisi kupitia akaunti yako ya SIPA (Student’s Individual Permanent Account). Hii ndiyo njia rasmi ya kuangalia majibu yako ya maombi ya mkopo.
Hatua za Kuangalia Majina ya Waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Pili kupitia SIPA:
- Tembelea Tovuti ya H E S L B:
https://olas.heslb.go.tz/olams/account/login - Ingia kwenye Akaunti Yako:
Tumia username na password uliotumia wakati wa kuomba mkopo. - Bofya “SIPA” kisha “ALLOCATION”
- Chagua Mwaka wa Masomo (2025/2026)
Hapa utaona kama umepewa mkopo na kiasi ulichopangiwa.
Kagua mara kwa mara kwa sababu taarifa zinaweza kubadilika wakati wowote.
Kumbuka
- Maamuzi ya mikopo hutolewa kwa awamu.
- Ikiwa hujaonekana kwenye orodha hii ya pili, unaweza kusubiri awamu ya tatu.
- Fuata taarifa rasmi kutoka HESLB kupitia tovuti yao au kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Angalia Hapa: Majina ya Waliopata Mkopo 2025/2026 HESLB
Be the first to comment