Matokeo ya Darasa la Nne 2024, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) hutoa matokeo ya mtihani wa Darasa la Nne mwishoni mwa mwezi Desemba au mwanzoni mwa mwezi Januari wa mwaka unaofuata. Ratiba hii hutegemea mchakato wa ukaguzi wa kina wa mitihani, uthibitishaji wa matokeo, na maandalizi ya kutangaza taarifa rasmi kwa umma. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa tarehe hizi zinaweza kubadilika kulingana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na zui la ufanisi katika zoezi la uhakiki wa mitihani.
Wazazi, walimu, na wanafunzi wanashauriwa kuwa makini na kufuatilia taarifa rasmi kupitia tovuti ya NECTA kwa anwani ya www.necta.go.tz, ili kuepuka taarifa zisizo rasmi au zisizo sahihi zinazoweza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne 2024 NECTA Baada ya Kutangazwa
Baada ya matokeo ya mtihani wa Darasa la Nne 2024 kutangazwa rasmi na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), wanafunzi, wazazi, na walimu wanaweza kutazama matokeo kwa urahisi kwa kufuata hatua zifuatazo:
Hatua za Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA
- Fungua kivinjari cha mtandao kwenye simu yako au kompyuta.
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kwa kutumia anwani: www.necta.go.tz.
- Bonyeza sehemu ya “RESULTS” inayopatikana kwenye menyu kuu.
- Chagua “Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) 2024”.
- Orodha ya mikoa yote ya Tanzania itajitokeza. Bonyeza jina la mkoa wako ili kufungua orodha ya wilaya zote.
- Chagua wilaya yako, kisha tafuta shule yako au kituo cha mtihani.
- Bonyeza jina la shule yako ili kuona matokeo ya wanafunzi wa shule hiyo.
Viungo vya Moja kwa Moja (Direct Links)
Tunakupa viungo vya moja kwa moja kwa kila mkoa, hivyo unaweza kufikia matokeo haraka zaidi bila usumbufu. Baada ya NECTA kutangaza matokeo, bonyeza jina la mkoa husika kutoka kwenye jedwali ili kuona matokeo ya shule zote zilizopo katika mkoa huo.
Kuelewa Matokeo ya Darasa la Nne 2024
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) hupanga matokeo kwa namna inayorahisisha ufahamu wa ufaulu wa wanafunzi katika masomo mbalimbali. Hapa tumekuletea muhtasari wa jinsi matokeo ya shule yatakavyoonekana baada ya kutangazwa.
Muundo wa Matokeo ya Darasa la Nne
Matokeo ya Darasa la Nne yanajumuisha vipengele vifuatavyo:
- Idadi ya Wanafunzi Walioshiriki Mtihani
Matokeo huonyesha jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani, idadi ya walioshiriki, na taarifa za wale ambao hawakuhudhuria. - Wastani wa Shule
Wastani wa alama ya shule yote hutolewa, ukionyesha kiwango cha jumla cha ufaulu wa wanafunzi wa shule husika. Hii pia inajumuisha daraja la wastani la shule, ambalo linaweza kuwa A, B, C, au D, kulingana na viwango vya ufaulu. - Madaraja ya Ufaulu
Matokeo yanatenganisha wanafunzi kulingana na madaraja yao ya ufaulu:- A: Sifa ya Juu
- B: Nzuri Sana
- C: Nzuri
- D: Inaridhisha
- Referred: Wanafunzi waliokosa vigezo vya ufaulu
- Matokeo ya Mwanafunzi Binafsi
Matokeo ya kila mwanafunzi huoneshwa kulingana na alama alizopata katika kila somo alilopimwa. Hapa huoneshwa:- Majina ya mwanafunzi na namba ya mtahiniwa.
- Alama za kila somo.
- Daraja lililopatikana kwa kila somo (kwa mfano, A, B, C, au D).
- Wastani wa alama za jumla na daraja la jumla kwa mwanafunzi.
- Ufaulu wa Masomo kwa Shule
Matokeo huonyesha muhtasari wa ufaulu wa masomo kwa shule nzima, ikijumuisha:- Idadi ya wanafunzi waliopata daraja tofauti (A-D).
- Wastani wa alama kwa kila somo.
- Daraja la wastani kwa kila somo.
Be the first to comment