Nafasi ya Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Moshi April 2025

Nafasi ya Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Moshi April 2025

POST : MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 1 POST

Mwajiri: Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
Muda wa Kuomba: Kuanzia tarehe 17 Aprili 2025 hadi 30 Aprili 2025
Mshahara: Kwa mujibu wa ngazi ya mishahara ya serikali – TGS.C

Maelezo ya Kazi

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi ya Katibu Mahususi. Hii ni nafasi muhimu inayohusisha shughuli mbalimbali za kiofisi kwa ajili ya kusaidia watendaji waandamizi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Majukumu ya Kazi

Miongoni mwa majukumu ya Katibu Mahususi ni:

  1. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali (za kawaida na za siri).
  2. Kupokea wageni, kusikiliza shida zao na kuwaelekeza mahali sahihi pa kupata msaada.
  3. Kutunza kumbukumbu muhimu kama matukio, miadi, tarehe za vikao na safari za mkuu wake.
  4. Kutafuta nyaraka na majalada yanayohitajika kwa ajili ya kazi.
  5. Kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa katika idara husika.
  6. Kuhifadhi na kurudisha majalada/nyaraka sehemu husika.
  7. Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.
  8. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
  9. Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Sifa za Mwombaji ¬ Nafasi ya Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Moshi

Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  • Awe amehitimu Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
  • Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili.
  • Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa kiwango cha maneno 100 kwa dakika moja.
  • Awe na mafunzo ya matumizi ya programu za kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher, kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.

TUMA MAOMBI HAPA

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*