
NAFASI YA KAZI: DEREVA WA GARI KUBWA AINA YA HOWO HORSE
IDADI YA NAFASI: Sita (06)
MAHALI PA KAZI: Bagamoyo
TAREHE YA TANGAZO: 06/05/2025
MAJUKUMU YA KAZI Bagamoyo Sugar
- Kuendesha gari kubwa kwa ajili ya kusafirisha miwa na kuhamisha mitambo.
- Kufata taratibu za kampuni kuhusu njia za kusafiri na ratiba za kupeleka mizigo.
- Kuzingatia sheria zote za usalama na sera za kampuni.
- Kuwa na uaminifu, kufika kwa wakati na kuhakikisha miwa inafikishwa kiwandani salama na kwa ufanisi.
- Kuhakikisha matatizo yote ya gari yanarekebishwa kabla ya kuanza safari.
- Kuripoti ajali, matatizo ya gari, au ukiukwaji wa sheria.
- Kufanya matengenezo ya kila siku ya gari kama kujaza mafuta na usafi wa gari.
SIFA ZA MWOMBAJI Bagamoyo Sugar
- Awe na uzoefu wa kuendesha gari la Howo Horse kwa muda wa angalau miaka 3.
- Awe na leseni ya daraja E iliyo hai pamoja na cheti halisi cha VETA.
- Awe Mtanzania na mwenye umri usiopungua miaka 18.
- Awe na kitambulisho cha NIDA na namba ya mlipa kodi (TIN).
- Awe na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa na barua za wadhamini wawili.
- Awe ametuma nyaraka zote kama PDF moja (file moja).
JINSI YA KUTUMA MAOMBI | Nafasi ya Kazi Udereva Bagamoyo Sugar
Tuma maombi yako kwa barua pepe ukitaja nafasi unayoomba kwenda: [email protected]
Mwisho wa kutuma maombi: 12/05/2025
ANGALIZO MUHIMU
Epuka rushwa. Ikiwa mtu yeyote atakuomba kitu kwa ahadi ya kukusaidia upate kazi, tafadhali ripoti kupitia:
📞 0677113947
📧 [email protected]
Be the first to comment