Nafasi za Kazi 4 Wilaya ya Mbeya 2025, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya anapenda kuwatangazia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kutuma maombi ya kuwa mjumbe wa Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri. Bodi inatokana na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura Na. 287. Bodi hiyo itakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu (3).
Wajumbe wanaohitajika (wanaopigiwa kura):
- Wawakilishi wa watumiaji Huduma za Afya (Jamii) wanne kati yao wawili ni wanawake (nafasi 4).
- Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Afya za jamii (nafasi 1).
- Mwakilishi kutoka watoa Huduma za Afya binafsi (nafasi 1).
- Mwakilishi kutoka Taasisi/Asasi za kijamii (Civil Society organization) watoa huduma za Afya (FBOs na NGOs) (nafasi 1).
Sifa za kuwa Mjumbe wa Bodi ya Huduma za Afya za Halmashauri:
- Awe ni Raia wa Tanzania.
- Awe na umri usiopungua miaka 21 na usizidi miaka 75.
- Awe na Elimu ya kuanzia kidato cha Nne na kuendelea.
- Awe na akili timamu.
- Awe mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
- Awe Mwanachama hai wa Mfuko wa Jamii (CHF/TIKA).
Jengo la Ofisi ya Halmashauri Iwindi, S.L.P. 599 Mbeya,
Simu: +255 734 189 769
Nukushi: +255-2500128
Barua pepe: [email protected]
Tovuti: www.mbeya
Nafasi za Kazi 4 Wilaya ya Mbeya ~ Nafasi za kazi Halmashauri

Be the first to comment