
Nafasi za kazi Bagamoyo Sugar: AFISA MANUNUZI NA UHIFADHI WA VIFAA
MAHALI: Bagamoyo
TAREHE: 04 Machi 2025
Majukumu na Wajibu:
- Kuhakikisha ubora na kiasi sahihi cha vifaa na bidhaa zinazopokelewa.
- Kudumisha rekodi sahihi za bidhaa na vifaa.
- Kupokea bidhaa kutoka kwa wasambazaji.
- Kuanzisha maombi ya ununuzi wa vifaa pale inapohitajika.
- Kusambaza vifaa kutoka stoo kwa watumiaji wa mwisho.
- Kuandaa ripoti za kila siku na kila mwezi.
Sifa na Ujuzi Unaohitajika
- Uzoefu wa kazi wa angalau miaka miwili katika nafasi inayofanana.
- Uwezo mzuri wa kuzungumza na kuandika kwa Kiswahili na Kiingereza.
- Uwezo mzuri wa kuwasiliana na kushirikiana katika shughuli za kila siku.
- Diploma katika Uhasibu, Fedha, Ununuzi na Usambazaji au fani inayohusiana.
Jinsi ya Kutuma Maombi: Nafasi za kazi Bagamoyo Sugar
- Waombaji wanakaribishwa kuwasilisha maombi yao kwa barua pepe [email protected], wakieleza jina la nafasi wanayoomba.
- Tarehe ya mwisho wa kutuma maombi ni: 14 Machi 2025.
Taarifa Muhimu:
Epuka vitendo vya rushwa! Endapo mtu yeyote atakudai chochote kwa ahadi ya ajira, tafadhali ripoti kupitia:
0677 113 947
[email protected]
Imetolewa na:
Ofisi ya Rasilimali Watu, Bagamoyo Sugar Limited.
Kwa Taarifa zaidi Bonyeza hapa
Be the first to comment