
Benki ya NMB ni moja ya benki kubwa zaidi za biashara nchini Tanzania, ikitoa huduma za kibenki kwa watu binafsi, wateja wa makampuni madogo na ya kati, huduma za serikali, biashara kubwa na mikopo ya kilimo. N M B ilianzishwa chini ya Sheria ya Kuanzishwa kwa Benki ya Taifa ya Huduma Ndogo za Kifedha ya mwaka 1997, kufuatia kugawanywa kwa Benki ya Biashara ya Taifa ya zamani kwa mujibu wa sheria ya Bunge. Wakati huo, taasisi tatu mpya ziliundwa:
(a) NBC Holdings Limited
(b) National Bank of Commerce (1997) Limited
(c) National Microfinance Bank Limited (NMB).
Kwa sasa, NMB ina matawi 226, mawakala zaidi ya 9,000 na zaidi ya mashine 700 za ATM kote nchini, ikiwa na uwakilishi katika kila wilaya ya Tanzania. Benki hii ina zaidi ya wateja milioni 4 na inaajiri wafanyakazi zaidi ya 3,400. NMB pia imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Wanahisa wakubwa wa benki hii ni Arise B.V (wanaomiliki 34.9% ya hisa) na Serikali ya Tanzania (inayomiliki 31.8% ya hisa).
Katika Tuzo za Ubora za Euromoney, N M B ilichaguliwa kuwa “Benki Bora Tanzania” kwa miaka 8 mfululizo kuanzia 2013 hadi 2020. Pia, Global Finance Magazine iliitaja NMB kama “Benki Salama Zaidi Tanzania” kwa mwaka 2020.
Nafasi za kazi Benki ya NMB
Benki inakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye sifa stahiki kujaza nafasi mpya za kazi.
SOMA MAELEZO KAMILI KUPITIA kiungo ILIYOAMBATANISHWA HAPA CHINI:
Nafasi: Meneja Mwandamizi Omba Hapa
Nafasi: Mchambuzi (Data Science) Omba Hapa
Angalia hapa: Nafasi za kazi CultivAid April 2025
Be the first to comment