
BRAC Maendeleo Tanzania ni sehemu ya shirika kubwa la maendeleo ambalo lilianza shughuli zake mwaka 2006 hapa Tanzania. Shirika hili linajikita zaidi katika maeneo ya Kilimo, Uwezeshaji wa Vijana na Wanawake, Usalama wa Chakula na Maisha Endelevu.
Mwaka 2022, Taasisi ya Mastercard kwa kushirikiana na BRAC International (BI) ilitangaza mpango maalum wenye lengo la kuleta mabadiliko chanya na yanayoweza kupimika kwa wasichana balehe na wanawake vijana wapatao milioni 1.2, pamoja na watu milioni 9.5 katika nchi saba za Afrika Mashariki na Magharibi. Nchi hizo ni Ghana, Kenya, Liberia, Rwanda, Sierra Leone, Tanzania na Uganda.
Kuna haja kubwa ya kuwasaidia wasichana balehe na wanawake vijana wanaoishi katika umaskini, hasa baada ya athari za janga la dunia la COVID-19. Kupitia ushirikiano huu, mbinu mbalimbali za kukuza maendeleo ya kiuchumi zitatolewa kwa jamii ili kuwapa uwezo na sauti wasichana hawa. Watapata nafasi ya kutimiza malengo yao, kujipatia maisha bora endelevu, na kushiriki katika masuala ya utetezi.
BRAC International itatekeleza mfumo wa pamoja na wa kina ili kushughulikia hatua mbalimbali za maisha ya msichana anayekua katika mazingira ya umaskini, kuhakikisha anapita salama kutoka kipindi cha balehe hadi utu uzima.
Shirika hili ni mwajiri anayetoa fursa sawa kwa wote.
Nafasi za Kazi BRAC Maendeleo Tanzania
Shirika linakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye sifa na uwezo kujaza nafasi mpya za kazi. SOMA MAELEZO KAMILI KUPITIA KIUNGANISHI ILIYO AMBATTANISHWA HAPA CHINI:
- Nafasi: Mkuu wa Rasilimali Watu na Mafunzo Omba Hapa
Be the first to comment