
NAFASI YA KAZI: FUNDI MEKANIKI
IDADI YA NAFASI: TATU (03)
MAHALI PA KAZI: BAGAMOYO
TAREHE: 06/05/2025
MAJUKUMU YA KAZI | Bagamoyo Sugar
- Kufanya uchunguzi wa kitaalamu wa matatizo ya magari (madogo na makubwa).
- Kufanya matengenezo na kubadilisha sehemu za magari inapohitajika.
- Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na matengenezo ya tahadhari kwa magari madogo na makubwa.
- Kupima utendaji wa magari.
- Kuwa na ujuzi wa kutumia vifaa vya uchunguzi wa magari.
- Kuhakikisha viwango vya usalama vinafuatwa.
- Kufanya kazi nyingine yoyote utakayopangiwa na wakubwa wako.
SIFA NA UJUZI UNAOHITAJIKA
- Awe na cheti cha Ufundi Magari (ngazi ya 3 au daraja la kwanza).
- Awe na uzoefu wa kazi wa miaka 5 au zaidi, hasa kwenye mazingira ya usafirishaji mizigo, ni vyema zaidi kama ana uzoefu kwenye viwanda vya sukari.
- Awe Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
- Awe na kitambulisho cha NIDA na namba ya mlipa kodi (TIN).
- Awe na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa na barua mbili za wadhamini.
- Awe ametuma nyaraka zote katika faili moja la PDF.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI | Nafasi za kazi Fundi Mechanic Bagamoyo Sugar
Tuma maombi yako ukieleza jina la nafasi unayoomba kupitia barua pepe:
📧 [email protected]
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12/05/2025.
MUHIMU: Epuka rushwa. Iwapo mtu yeyote atakuomba kitu kwa ahadi ya kukupatia kazi au kukusaidia upate kazi, tafadhali toa taarifa kupitia namba: 0677113947 au barua pepe: [email protected]
Be the first to comment