Nafasi ya Kazi: Fundi wa Zana za Kilimo (Implement Mechanic)
Nafasi wazi: Moja (1)
Mahali pa kazi: Bagamoyo
Tarehe ya tangazo: 03/05/2025
Majukumu/Majibu:
- Kuhakikisha usalama katika mazingira ya kazi.
- Kuhakikisha usafi wa sehemu ya kazi.
- Kuwajibika katika matengenezo na marekebisho ya zana/mashine za kilimo.
- Kubaini matatizo (hitilafu) katika zana/mashine za kilimo.
- Kuhakikisha usalama na usafi wakati wa kufanya kazi.
- Kufanya huduma (service) za zana pamoja na kusaidia katika kuagiza vipuri.
- Kufanya majukumu mengine yoyote atakayopewa na Mkuu wa Idara (HOD-WS).
Sifa na Ujuzi Unaohitajika:
- Cheti cha Juu (Advanced Certificate) katika teknolojia ya magari au Diploma ya mitambo ya kilimo (Agro mechanics).
- Uzoefu wa angalau miaka 3 katika kutunza na kutengeneza zana za kilimo.
- Mwombaji lazima awe na NIDA (kitambulisho cha Taifa) na TIN (namba ya mlipa kodi).
- Mwombaji anatakiwa kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa na barua mbili za marejeo (referees).
- Hati zote za uthibitisho (vyeti na nyaraka) zitumwe kama faili moja la PDF. Kutokufuata utaratibu huu kutafanya maombi yakataliwe.
Jinsi ya Kutuma Maombi: Nafasi za kazi Fundi wa Zana za Kilimo Bagamoyo Sugar
Tuma maombi yako ukieleza nafasi unayoomba kupitia barua pepe: [email protected]
Mwisho wa kutuma maombi: 08/05/2025
Tangazo limetolewa na Ofisi ya Rasilimali Watu, Bagamoyo Sugar Limited.
Angalizo Muhimu:
Epuka rushwa. Ikiwa mtu yeyote atakuomba rushwa kwa ahadi ya kukusaidia kupata kazi, tafadhali ripoti kupitia namba: 0677 113 947 au barua pepe: [email protected].
Be the first to comment