
Nafasi za kazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Nafasi ya Kazi: Dereva Daraja II – Nafasi 1
Mwajiri: Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Muda wa Maombi: 28 Aprili 2025 – 12 Mei 2025
Maelezo ya Kazi
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi ya Dereva Daraja II.
Majukumu ya Msingi:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwa safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari.
- Kutekeleza majukumu mengine atakayoelekezwa na Msimamizi wake.
Sifa za Mwombaji Nafasi za kazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
- Awe na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari na awe ameendesha kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehitimu Mafunzo ya Msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara
- Mshahara unatolewa kwa Mujibu wa Ngazi ya Mishahara ya Serikali – TGS B.
Be the first to comment