
Mkaguzi wa Ndani (Internal Auditor)
Majukumu Muhimu:
- Kuhakikisha magari yanakidhi viwango vya usalama, mazingira (emissions), na ubora wa kutumika barabarani kama vinavyotakiwa na mamlaka husika.
- Kufanya ukaguzi kwa kutumia orodha ya ukaguzi (audit checklist) iliyotolewa.
- Kazi zote za ukaguzi zitekelezwe kulingana na muda uliopangwa kwenye ratiba ya kazi/ukaguzi.
- Kuandaa ripoti ya ukaguzi kwa kutumia kiolezo rasmi cha ripoti (Audit Report Template).
- Kila ukaguzi lazima uandaliwe kwa kutumia taarifa za ukaguzi za Mwaka hadi Sasa (Year to Date) pamoja na viambatisho (Annexure).
- Taarifa zote za ukaguzi, viambatisho, na ripoti ziwekwe majina wazi kwa matumizi ya baadae kwenye ukaguzi unaofuata.
- Kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa marekebisho ya mapungufu yaliyoonekana kwenye ukaguzi, kwa kushirikiana na wakuu wa idara au vitengo husika.
- Kufanya ukaguzi kwa niaba ya wenzako endapo watakuwa likizo au wamepewa majukumu mengine katika vituo vingine.
- Kushiriki kwenye miradi mingine au majukumu yoyote utakayopangiwa, pamoja na kuhudhuria mikutano ya timu.
Sifa za Mwombaji:
- Shahada ya kwanza ya Uhasibu, Fedha au fani inayohusiana, pamoja na CPA.
- Uwezo mzuri wa kuchambua taarifa na kuandika ripoti.
- Uadilifu wa hali ya juu, uwezo wa kutunza siri, na makini kwa undani.
- Ujuzi mzuri wa kutumia mifumo ya kihasibu kama Tally, QuickBooks, Sage n.k.
- Uzoefu: Angalau mwaka 1 katika kazi zinazohusiana na ukaguzi wa magari, matengenezo ya magari, au ukaguzi wa ndani/wa nje.
- Mahali pa kazi: Moshi.
Jinsi ya Kutuma Maombi: Nafasi za kazi Internal Auditor Bonite
Hii ni kazi ya muda wote. Maombi yote yaambatane na barua ya maombi, nakala za vyeti, na wasifu (CV), yatumiwe kwa barua pepe [email protected] au kwa anuani hapa chini, ili yafikie ofisini kabla ya tarehe 19/05/2025.
Mkurugenzi Mtendaji,
Bonite Bottlers Ltd,
S.L.P. 1352,
Moshi.
Be the first to comment