
4 Nafasi za kazi PASS Trust April 2025, PASS Trust ni taasisi iliyoanzishwa mwaka 2000 kwa ajili ya kuchochea uwekezaji na ukuaji katika kilimo cha kibiashara na sekta zinazohusiana. Ilisajiliwa rasmi mwaka 2007 kama taasisi isiyo ya kiserikali na isiyo ya faida, chini ya Sheria ya Usajili wa Wadhamini ya mwaka 2002, na inatambuliwa kama taasisi ya hisani kwa upande wa kodi.
Dira ya PASS: Kuwa taasisi ya ubunifu ya maendeleo ya fedha kwa kilimo inayoboresha maisha ya wajasiriamali wadogo wa kilimo.
Dhamira ya PASS: Kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na maendeleo ya biashara kwa wajasiriamali wa kilimo hapa Tanzania.
Kupitia huduma ya ukodishaji wa vifaa (leasing), PASS inamuwezesha mjasiriamali kupata vifaa au mashine bila kulipa fedha zote kwa wakati mmoja. Muuzaji wa vifaa hupokea malipo yake, wakati mjasiriamali huendelea kulipa kidogo kidogo kwa awamu walizokubaliana. Huduma hii inalenga kusaidia wale wanaotaka kuanzisha au kukuza biashara zao za kilimo lakini hawana mitaji ya kutosha ya kununua vifaa au mashine.
Lengo kuu la PASS Leasing ni kufadhili wajasiriamali wadogo na wa kati katika sekta ya kilimo kupitia ukodishaji wa mashine na vifaa vinavyohusiana na mnyororo mzima wa thamani wa kilimo—ikiwemo mazao, mifugo, uvuvi, misitu na ufugaji wa nyuki.
PASS ni mwajiri anayetoa fursa sawa kwa wote, hivyo waombaji wote wenye sifa wanahamasishwa kutuma maombi.
Nafasi za kazi PASS Trust
Kampuni inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania kujaza nafasi mpya za ajira.
SOMA MAELEZO KAMILI KUPITIA LINK HAPO CHINI:
Be the first to comment