Nafasi za kazi TAHA May 2025

Nafasi za kazi TAHA May 2025

Nafasi za kazi TAHA, TAHA ni chama cha sekta binafsi chenye wanachama, ambacho kimepewa jukumu la kuendeleza na kukuza sekta ya kilimo cha bustani nchini Tanzania. Hii inajumuisha maua, matunda, mboga, viungo, mimea tiba na mbegu za bustani.

Lengo kuu la TA.HA ni kukuza ukuaji na ushindani wa sekta ya bustani ili kuleta manufaa ya kijamii na kiuchumi. TA,HA pia ni jukwaa la pamoja linalowakilisha wakulima wa ngazi zote, wasindikaji, wauzaji wa nje na watoa huduma kwenye sekta ya bustani nchini.

Kwa sasa, TAHA inatekeleza mradi wa miaka mitano unaofadhiliwa na USAID uitwao “USAID Tuhifadhi Chakula.” Mradi huu unalenga kupunguza upotevu wa chakula baada ya mavuno kwa kuboresha njia za kuhifadhi na kushughulikia mazao katika mnyororo wa thamani. Lengo ni kuongeza usalama wa chakula nchini.

Mradi unajikita kwenye maeneo makuu manne:

  1. Kuboresha usimamizi wa mazao baada ya kuvunwa (kama vile uhifadhi na usindikaji) kwa wakulima na wafanyabiashara.
  2. Kuwezesha upatikanaji wa masoko ili bidhaa za kilimo ziwafikie walaji.
  3. Kusaidia utungaji wa sera na kanuni zitakazopunguza upotevu wa chakula.
  4. Kuijengea uwezo taasisi za ndani kuongoza masuala ya usimamizi wa mazao baada ya mavuno.

TAHA ni mwajiri anayetoa fursa sawa kwa wote, hivyo inawahamasisha waombaji wote wenye sifa kuwasilisha maombi.

Nafasi za kazi TAHA

Taasisi inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kuomba nafasi hii mpya ya kazi.
SOMA MAELEZO KAMILI HAPO CHINI:

  1. Nafasi: Msaidizi wa Mahusiano ya Wateja Omba Hapa

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*