
Kichwa cha Nafasi: Dereva Daraja II (Nafasi 1)
Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Same
Muda wa Maombi: 2 Mei 2025 hadi 11 Mei 2025
Muhtasari wa Kazi: Hakuna
Majukumu ya Kazi:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake
Sifa na Uzoefu:
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya daraja E au C ya uendeshaji magari, ambayo ameifanyia kazi kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Pia awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.
Mshahara: TGS B
Nafasi za kazi Udereva Halmashauri ya Wilaya ya Same
Angalia Hapa: Jinsi ya Kujisajili na Ajira Portal
Be the first to comment