
Nafasi za kazi Udereva Hyperlink Logistics
Nafasi ya Kazi: Dereva wa Pikipiki kwa Ajili ya Kusafirisha Mizigo
Mahali: Dar es Salaam, Tanzania
Tarehe ya Kuanza: Juni 2025
Aina ya Mkataba: Kazi ya muda wote (Full-time)
Kuhusu Kampuni Yetu:
Hyperlink Logistics ni kampuni mpya katika sekta ya usafirishaji, inayolenga kuziba pengo lililopo kwa kutoa suluhisho za kisasa kwa wateja kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa na timu changa, yenye bidii na ari kubwa ya kazi. Makao makuu yapo Dar es Salaam, Tanzania.
Majukumu Makuu ya Nafasi hii:
- Kukagua oda kabla na baada ya kuwasilisha kuhakikisha zimekamilika, malipo ni sahihi, na mteja ameridhika.
- Kupakia, kusafirisha na kuwasilisha mizigo kwa wateja kwa usalama na kwa wakati.
- Kutoa huduma bora kwa wateja, kujibu maswali na kushughulikia malalamiko.
- Kufata njia zilizopangwa na ratiba za muda.
- Kuheshimu sheria zote za usafiri na kudumisha rekodi nzuri ya udereva.
- Kuandaa ripoti na nyaraka nyingine zinazohusu usafirishaji.
- Kuendesha vifaa kama vile pikipiki na magari.
- Kuwa na uwezo wa kujisimamia, kuwa mkweli na kufanya kazi bila kusimamiwa kila wakati.
- Kujenga na kuimarisha mahusiano bora na wateja ili kuongeza thamani kwa biashara yao.
- Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na uongozi.
Sifa za Mwombaji:
- Awe amehitimu elimu ya sekondari.
- Awe na leseni halali ya kuendesha pikipiki na magari.
- Awe na rekodi safi ya udereva.
- Awe anazijua vizuri barabara, mitaa na maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.
- Awe na uwezo mzuri wa kusimamia muda na kuhudumia wateja.
- Awe na tabia nzuri na uwezo wa kushirikiana na watu wengine.
- Awe na uwezo wa kupakia na kushusha mizigo.
Jinsi ya Kuomba: Nafasi za kazi Udereva Hyperlink Logistics
Tuma CV yako na barua ya maombi kwenda kwa: [email protected]
Angalizo: Ni waombaji waliopitishwa tu watakaowasiliana nao.
Mwisho wa Kutuma Maombi: 15 Mei 2025
Be the first to comment