Nafasi za kazi Uhasibu TANROADS April 2025

Nafasi za kazi Uhasibu TANROADS April 2025, Nafasi za kazi Afisa Mizani TANROADS April 2025, Nafasi za kazi Udereva TANROADS April 2025

WAKALA WA BARABARA TANZANIA (TANROADS) ni taasisi ya serikali inayohusika na matengenezo na uendelezaji wa barabara kuu katika Tanzania Bara. Pia inasimamia miundombinu ya barabara katika mikoa mbalimbali.

Meneja wa Mkoa – TANROADS Mkoa wa Pwani, kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki na uwezo wa kujaza nafasi zifuatazo kwa mkataba wa muda maalum (unaoweza kuhuishwa):

Nafasi: Msaidizi wa Hesabu Daraja la Kwanza – Nafasi 2

Sifa za Kujiunga:
Mwombaji anatakiwa awe na Stashahada ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambulika au awe na Cheti cha Accounting Technician Certificate II (ATEC II) kinachotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) au sifa nyingine zinazotambulika na NBAA.

Majukumu ya Kazi:

  • Kuandaa na kutoa hundi.
  • Kukusanya mapato.
  • Kuandaa malipo.
  • Kufanya upatanisho wa taarifa za benki.
  • Kushughulikia na kurekodi miamala ya kifedha.
  • Kushughulikia malipo ya mishahara na ujira.
  • Kutunza na kusasisha daftari la mali zisizohamishika.
  • Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopewa na msimamizi wake.

Mshahara: Ngazi ya mshahara TRDS 4.1

Masharti ya Jumla: Nafasi za kazi Uhasibu TANROADS

  • Waombaji ni lazima wawe Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
  • Watu wenye ulemavu wanahimizwa sana kutuma maombi na wanatakiwa kuonyesha hali hiyo kwenye mfumo wa Sekretarieti ya Ajira kwa Umma kwa ajili ya kupewa kipaumbele.
  • Waombaji wambatishe wasifu wa kisasa (CV) wenye mawasiliano sahihi: anuani ya posta, baruapepe, na namba za simu.
  • Maombi yafanywe kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa katika tangazo hili.
  • Waombaji waambatishe nakala zilizoidhinishwa za vyeti vifuatavyo:
    • Vyeti vya Shahada/Stashahada/Vyeti vya kozi husika;
    • Matokeo ya Shahada/Stashahada;
    • Vyeti vya Kidato cha Nne (Form IV) na Kidato cha Sita (Form VI);
    • Cheti cha kuzaliwa.

Vyeti vifuatavyo havitakubaliwa:

  • Slips za matokeo ya Kidato cha Nne na Sita;
  • Testimonials na matokeo yasiyokamilika (partial transcripts).
  • Mwombaji ambaye tayari ni mtumishi wa umma kwa ajira ya kudumu na inayolipwa pensheni anatakiwa kuonyesha hali hiyo.
  • Wataje waamuzi watatu wa kuaminika na mawasiliano yao kamili.
  • Vyeti vya elimu kutoka nje ya nchi vinatakiwa kuthibitishwa na NECTA (kwa elimu ya sekondari) na NACTE (kwa vyuo vya elimu ya juu).

📅 Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 07 Mei, 2025.

⚠️ Kuwasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo kutasababisha hatua kali za kisheria.

✅ Ni waombaji waliopata nafasi ya usaili pekee ndio watakaojulishwa tarehe ya usaili.

Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na ipelekwe kwa:

Meneja wa Mkoa
TANROADS
S.L.P. 30150
KIBAHA – PWANI

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*