
Nafasi: Wakala wa Mauzo (Sales Freelancers)
Maelezo:
Kampuni ya The Guardian Limited inatafuta wakala wa mauzo wenye juhudi binafsi (freelancers) kujiunga na timu yao ya Mauzo ya Matangazo katika mikoa ya Arusha, Tanga, Morogoro, Iringa, Mbeya, Mwanza, na Kilimanjaro.
Majukumu:
- Kuwatafuta wateja wapya kwa bidii na kukuza biashara iliyopo.
- Kubuni njia mpya za kupata wateja.
- Kutengeneza na kufuatilia mipango ya biashara ili kuhakikisha mauzo yanakua.
- Kutoa suluhisho za kimkakati kulingana na mahitaji ya kila mteja.
Sifa za Muombaji:
- Awe na uwezo wa kufikia malengo yaliyowekwa kwa wakati katika mazingira ya ushindani kazini.
- Awe na mpangilio mzuri, mwenye motisha ya ndani, mtazamo chanya na anayependa kufanikisha malengo mapya.
- Awe na cheti cha diploma au shahada ya chuo kikuu katika Utawala wa Biashara (Business Administration).
- Uzoefu katika mauzo na masoko utapewa kipaumbele.
Angalizo:
Hii ni nafasi ya kazi ya malipo kwa tume (commission-based) – si mshahara wa kila mwezi.
Jinsi ya Kuomba: Nafasi za Kazi Wakala wa Mauzo The Guardian Limited
Tuma maombi yako kwa barua pepe kupitia [email protected] kabla ya tarehe 15 Mei, 2025.
Be the first to comment