
Nafasi za Kazi WFP: Afisa Sera wa Mpango – Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi katika WFP:
Mwisho wa kutuma maombi:
30 Aprili 2025, saa 5:59 usiku – Saa za Afrika Mashariki (GMT+03:00, Dar es Salaam)
KUHUSU WFP
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ndilo shirika kubwa zaidi la kibinadamu duniani linalookoa maisha wakati wa dharura na kutumia msaada wa chakula kama njia ya kujenga amani, utulivu na ustawi kwa watu waliokumbwa na migogoro, majanga, na athari za mabadiliko ya tabianchi.
WFP inaamini katika utofauti na usawa kazini, na inahimiza watu wote wenye sifa kutuma maombi bila kujali rangi, asili, jinsia, imani, hali ya afya au ulemavu.
🔗 Tembelea: https://www.wfp.org
KWANINI UJIUNGE NA WFP?
- Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2020
- Mazingira ya kazi yenye utofauti na ushirikiano wa tamaduni mbalimbali
- Mafunzo na fursa za kukuza taaluma
- Fursa ya kufanya kazi kimataifa
- Mshahara na marupurupu ya kuvutia
MALENGO YA NAFASI HII YA KAZI
Mpango wa Uhimilivu wa Tabianchi wa WFP Tanzania unatekelezwa chini ya Mpango wa Kuwezesha Nchi (CSP 2022–2027), kwa lengo la kusaidia jamii na taasisi za ndani kujenga uwezo wa kustahimili na kukabiliana na uharibifu wa mazingira pamoja na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ni pamoja na:
- Kusaidia familia zisizo na usalama wa chakula kujenga mali na kutumia mbinu za kilimo zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi
- Kuimarisha uwezo wa serikali na wadau wengine kupitia usimamizi wa mabonde
- Kuwezesha utekelezaji wa kilimo kinachozingatia tabianchi (climate-smart agriculture)
MAJUKUMU MAKUU YA NAFASI
- Ubunifu na Mipango ya Uundaji Mali na Riziki
- Kuongoza mbinu endelevu za usimamizi wa maliasili, udongo, maji na mazingira
- Kuweka mikakati ya kudumu kwa ajili ya maeneo yaliyo hatarini kwa majanga kama ukame, maporomoko, na mafuriko
- Kuhakikisha jinsia na lishe vinaangaziwa katika mipango
- Mikakati ya Programu, Mazungumzo ya Sera na Uratibu wa Utekelezaji
- Kufuatilia utekelezaji wa kazi za umma zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi
- Kushirikiana na serikali, taasisi za utafiti na mashirika yasiyo ya kiserikali
- Kusaidia muunganiko kati ya hifadhi ya jamii, kilimo, lishe na hatua za utangulizi za kupunguza athari za majanga
- Uandishi wa Ripoti na Usimamizi wa Maarifa
- Kuandaa nyaraka na ushahidi wa utekelezaji wa programu
- Kutathmini mafanikio na changamoto katika utekelezaji
- Kushiriki mafunzo na maarifa bora kwa wadau mbalimbali
SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu
- Shahada ya Uzamili (Master’s) katika sayansi ya udongo, jiografia, usimamizi wa mazingira, kilimo, au taaluma zinazohusiana.
- Shahada ya kwanza inakubalika ikiwa na uzoefu wa ziada wa miaka 2.
Uzoefu
- Miaka 8–10 ya uzoefu wa kitaalamu baada ya kuhitimu katika masuala ya maendeleo vijijini, usimamizi wa mazingira, kilimo kinachozingatia tabianchi, n.k.
- Uwezo wa kufanya kazi na serikali, kutoa ushauri wa sera, kushirikiana na wadau mbalimbali
- Uzoefu wa kazi katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ni faida
Ujuzi wa Kiufundi
- Kuandaa miradi ya kijamii kwa kushirikisha wadau mbalimbali
- Kuandaa ripoti, muhtasari na nyaraka za kiufundi kwa lugha rahisi
- Uzoefu wa mafunzo na uratibu wa kazi za kitaifa/kijamii
- Uwezo wa kutumia programu za kompyuta (Word, Excel, PowerPoint)
Lugha
- Uwezo mzuri wa kuzungumza na kuandika Kiingereza
- Maarifa ya lugha ya Kiswahili ni faida
MUDA WA MKATABA:
Miezi 11
JINSI YA KUTUMA MAOMBI | Nafasi za Kazi WFP
- Tafadhali bofya kiungo hapa chini kutuma maombi:
🔗 BOFYA HAPA KUOMBA KAZI
⚠ WFP haidai ada yoyote katika mchakato wa ajira. Usijibu ujumbe wowote unaodai malipo kwa ajili ya kazi.
Angalia Hapa: Nafasi za kazi Tindwa Medical and health service April 2025
Be the first to comment