
Nafasi za Kazi za Ualimu Neema International, Neema International inatafuta walimu wawili wenye ari, weledi, na uzoefu kujiunga na timu yetu ya walimu wa shule ya msingi ya juu (Upper Primary).
Nafasi Zinazopatikana:
- Mwalimu wa Kiingereza – Shule ya Msingi ya Juu
- Mwalimu wa Sayansi – Shule ya Msingi ya Juu
Sifa za Jumla kwa Waombaji Wote:
- Awe na shahada ya ualimu (B.Ed au B.ECE)
- Awe na uzoefu wa kufundisha darasa la 4 hadi la 7
- Awe na uwezo mzuri wa kusimamia darasa na mawasiliano
- Awe na hamasa ya kutumia mbinu shirikishi na zinazomhusisha mwanafunzi moja kwa moja (student-centered, inquiry-based learning)
- Awe tayari kujifunza na kushirikiana na walimu wengine mara kwa mara
Sifa Maalum kwa Kila Nafasi:
Mwalimu wa Kiingereza:
- Uwezo mzuri wa kufundisha kusoma, kuandika, sarufi, na uelewa wa kusoma (reading comprehension)
- Uwezo wa kuingiza fasihi na uandishi wa ubunifu kwenye mtaala
Mwalimu wa Sayansi:
- Uelewa mzuri wa mtaala wa sayansi kwa shule ya msingi
- Uzoefu wa kutumia majaribio ya vitendo na mbinu za uchunguzi (inquiry-based instruction)
- Uwezo wa kuamsha fikra za kisayansi na udadisi kwa wanafunzi
Tunachotoa:
- Mazingira mazuri na ya kushirikiana kazini
- Fursa za mafunzo na kukuza taaluma
- Vifaa na rasilimali za kisasa za kufundishia
- Mshahara mzuri kulingana na uzoefu na sifa
Namna ya Kutuma Maombi: Nafasi za Kazi za Ualimu Neema International
Tuma CV yako, barua ya maombi (ikieleza wazi nafasi unayoomba), nakala za vyeti na majina ya refferees kwa: [email protected]
🗓 Mwisho wa kutuma maombi: 29/04/2025
Be the first to comment