Unakaribishwa katika jukwaa hili maalum lenye makala yenye jina la: Namna ya kuangalia namba ya nida Online Pdf 2024 (Njia za Kuangalia Namba ya NIDA Mtandaoni 2024). Makala hii imetoa majibu yote ya maswali yako kuhusu kutazama namba ya nida online nchini Tanzania.
Kuhusu Namna ya kuangalia namba ya nida Online Pdf 2024
National Identification Authority (NIDA) /Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni chombo cha kusimamia Vitambulisho vya Taifa nchini Tanzania.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ina jukumu la usajili na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na Kisheria. Wakazi halali wanastahiki kadi ya NIDA ikiwa wana kibali halali cha mkazi na pasipoti halali isiyopungua miezi sita.
Wazo la kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilizaliwa mwaka 1968 katika kikao cha “Interstate Intelligence Gathering” kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia.
Kwa wakati huo nchi za Kenya na Zambia tayari zilikuwa na Vitambulisho vyao vya Taifa. Iliazimiwa kwamba ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne ni lazima nchi za Uganda na Tanzania nazo zikatoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wao.
Jinsi ya Kuangalia Namba ya NIDA Online 2024
Kuangalia namba ya NIDA mtandaoni ndio njia rahisi, ya haraka, na ya kuaminika zaidi ikilinganishwa na njia zingine kama vile SMS na USSD. Kupitia mtandao, unaweza kupata namba yako bila makato yoyote na kwa uhakika zaidi. Ili kuangalia namba ya NIDA mtandaoni, unahitaji simu janja au kompyuta yenye uwezo wa kuunganishwa na intaneti.
Njia za Kuangalia Namba ya NIDA Online Mtandaoni 2024
Hapa kuna njia rahisi za kuangalia namba ya NIDA mtandaoni:
1. Tembelea Tovuti Rasmi:
Fungua kivinjari chako cha wavuti na uende kwenye tovuti rasmi ya NIDA: https://services.nida.go.tz/
2. Toa Taarifa Zinazohitajika:
Jaza kwa usahihi taarifa zifuatazo:
- Jina la kwanza
- Jina la mwisho
- Tarehe ya kuzaliwa
- Jina la kwanza la mama
- Jina la mwisho la mama
3. Thibitisha Wewe Sio Roboti:
Andika neno linaloonyeshwa kwenye picha ili kuthibitisha kuwa wewe si roboti.
4. Pata Namba ya NIDA:
Bofya kitufe cha “Angalia” ili kupata namba ya NIDA.
Je Umefurahia makala hii? toa maoni yako hapa chini, uliza swali lako kwa kutuandikia ujumbe kuhusu Namna ya kuangalia namba ya nida pdf download au mengineyo.
Be the first to comment