
Orodha ya Sikukuu za Kitaifa Tanzania 2025, Katika maisha ya haraka ya kila siku, ni rahisi kusahau siku za mapumziko ya kitaifa Tanzania. Usiamke asubuhi ukaenda kazini kumbe leo ni sikukuu ya taifa! Mwongozo huu utakusaidia kukumbuka kila siku kuu ya kitaifa kwa mwaka 2024 — kwa urahisi na haraka.
Kwa nini Sikukuu za Kitaifa Tanzania ni Muhimu?
- Ni zaidi ya mapumziko. Sikukuu hizi hutukumbusha historia, utamaduni, na maadili yanayotufanya kuwa Watanzania.
- Ni fursa ya kusherehekea mafanikio yetu. Kuanzia vita vya uhuru hadi mafanikio ya kiuchumi na kijamii, kila siku kuu inasimulia safari ya taifa letu.
- Ni wakati wa kuungana. Tunapokumbuka watu waliotutangulia, tunajifunza mshikamano na uzalendo.
Orodha ya Sikukuu za Kitaifa Tanzania 2025
Sikukuu | Tarehe | Maelezo |
---|---|---|
Siku ya Mwaka Mpya | 1 Januari | Mwanzo wa mwaka mpya, maadhimisho na maazimio mapya. |
Mapinduzi ya Zanzibar | 12 Januari | Kumbukumbu ya mapinduzi ya 1964. |
Ijumaa Kuu | 29 Machi (Ijumaa) | Kumbukumbu ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. |
Jumatatu ya Pasaka | 22 Aprili (Jumatatu) | Maadhimisho baada ya Pasaka. |
Siku ya Karume | 7 Aprili | Kumbukumbu ya Sheikh Abeid Amani Karume. |
Eid al-Fitr | 1 Aprili | Mwisho wa Ramadhani kwa Waislamu. |
Mapumziko ya Eid al-Fitr | 11 Aprili (Alhamisi) | Mapumziko ya ziada baada ya Eid. |
Siku ya Muungano | 26 Aprili | Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964). |
Siku ya Wafanyakazi | 1 Mei | Kuwaenzi wafanyakazi wa Tanzania. |
Eid al-Adha | 16 Juni | Kumbukumbu ya kujitolea kwa Ibrahim. |
Saba Saba | 7 Julai | Maadhimisho ya kuanzishwa kwa CCM. |
Nane Nane | 8 Agosti | Siku ya wakulima na wafugaji. |
Maulid Nabi | 15 Septemba | Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W). |
Siku ya Nyerere | 14 Oktoba | Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere. |
Siku ya Uhuru | 9 Desemba | Uhuru wa Tanganyika (1961). |
Krismasi | 25 Desemba | Kuzaliwa kwa Yesu Kristo. |
Siku ya Zawadi | 26 Desemba | Siku ya zawadi, baada ya Krismasi. |
Kumbuka: Tarehe za Eid al-Fitr, Eid al-Adha na Maulid Nabi zinaweza kubadilika kutokana na muandamo wa mwezi.
Angalia Hapa: Mwongozo wa JWTZ Vyeo Na Mishahara 2025
Be the first to comment