Tetesi za Usajili Dirisha Dogo limeanza kwa mvuto mkubwa, huku tetesi zikihusu wachezaji wapya na mipango ya kuimarisha vikosi vya timu kubwa za Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Hebu tuangalie tetesi hizi kwa undani!
Tetesi za Usajili
Simba SC
Simba inajipanga vikali kwa dirisha hili la usajili. Haya ni majina yanayozungumziwa:
- Tandi Mwape kutoka TP Mazembe na Feisal Salum wanatajwa kuwa kwenye rada za Simba.
- Aishi Manula, ambaye kwa sasa yuko Azam FC, huenda akarudi Simba kwa mkopo.
- Mshambuliaji kutoka Gambia, Foday Trawally, na beki Khadim Diaw, pia wanahusishwa na klabu hii.
Young Africans (Yanga SC)
Yanga nao hawabaki nyuma, wakilenga kuongeza nguvu kikosini:
- Wanamnyatia Karim Kimvuid kutoka TP Mazembe.
- Wanamtazama pia Duke Abuya wa Singida Black Stars, kama mbadala wa wachezaji ambao huenda wakaondoka.
- Israel Mwenda Kwenda Yanga ni DEAL DONE
Azam FC
Azam inatafuta kufanya mabadiliko makubwa:
- Wanatajwa kuwafukuzia Abutwalib Mshery na Aziz Ki ili kuimarisha safu yao.
Singida Black Starz
Singida Fountain Gate inazidi kujijenga:
- Wanaonyesha nia ya kuvutia wachezaji kutoka timu kubwa, hatua inayoweka klabu hiyo kwenye ramani ya usajili wa msimu huu.
- Klabu ya Singida Black Stars imeanza kujiimarisha mapema, ikitajwa tayari imemalizana na mshambuliaji, Jonathan Sowah raia wa Ghana kutoka Al Nasr Benghazi ya Libya.
- Klabu ya Singida Black Stars imefikia makubaliano na aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Miguel Angel Gamondi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Tahadhari kwa Klabu
Wataalamu wa michezo wanatoa onyo kali:
- Klabu zinashauriwa kuwa makini na mikataba ya wachezaji ili kuepuka matatizo ya kisheria, kama yale yaliyowahi kuzikumba Simba, Yanga, na Tabora United katika siku za nyuma.
Je, Nini Maoni Yako?
Mashabiki, ni wachezaji gani ungependa kuona katika kikosi chako? Tuambie mawazo yako! Endelea kufuatilia habari za usajili kwa updates za haraka na za kuaminika.
(Kwa maelezo zaidi, hakikisha unatembelea tovuti yetu kila siku!)
Be the first to comment