
Baada ya hatua ya robo fainali ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup, viwango vipya vya vilabu bora Afrika 2025 vimetangazwa rasmi.
Katika orodha hii ya vilabu 30 bora Afrika, klabu ya Simba SC kutoka Tanzania imeonyesha maendeleo makubwa. Simba imepanda kutoka nafasi ya 5 hadi nafasi ya 4 – ishara kuwa bado ni moja ya timu tishio barani Afrika.
Kwa upande mwingine, Yanga SC (Young Africans), ambao ni wapinzani wakubwa wa Simba, wameendelea kushikilia nafasi ya 11 kama ilivyokuwa awali.
Orodha Kamili ya Vilabu 30 Bora Afrika 2025
Hii hapa ni orodha ya vilabu bora kwa mujibu wa viwango vya CAF hadi kufikia hatua ya robo fainali ya mashindano ya kimataifa ya Afrika:
- Al Ahly
- Mamelodi Sundowns
- Esperance
- Simba SC
- Zamalek
- RS Berkane
- Wydad Casablanca
- Pyramids FC
- USM Alger
- CR Belouizdad
- Young Africans (Yanga SC)
- ASEC Mimosas
- Al Hilal
- TP Mazembe
- Orlando Pirates
- Raja Casablanca
- Petro de Luanda
- AS FAR Rabat
- MC Alger
- Sagrada Esperança
- CS Constantine
- Stellenbosch
- Al Masry
- Rivers United
- JS Kabylie
- Dreams FC
- Stade Malien
- Horoya AC
- Future FC
- Étoile du Sahel

Tanzania Yawakilishwa Vyema
Ni wazi kuwa Tanzania inaendelea kujivunia kuwa na vilabu viwili kwenye orodha hii ya vilabu bora Afrika – jambo ambalo linaonyesha maendeleo ya soka la nyumbani. Simba na Yanga zinaendelea kuweka alama kwenye ramani ya soka Afrika.
Angalia Hapa: Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025
Be the first to comment