
Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2024/2025 imetupa msimu wenye burudani safi na ushindani wa hali ya juu, hasa linapokuja suala la watoa asisti bora NBC Premier League 2024/2025. Katika kila mchuano, tumeshuhudia viungo na washambuliaji mahiri kutoka klabu kubwa kama Simba SC, Yanga SC, Azam FC na nyingine wakitengeneza nafasi hatari za mabao kwa ubunifu mkubwa.
Kwa Nini Watoa Asisti ni Muhimu?
Katika soka, asisti ni pasi ya mwisho inayomuwezesha mchezaji kufunga bao. Hii ina maana kwamba mchezaji anayetoa assist ni kiungo muhimu kati ya safu ya kiungo na washambuliaji. Uwezo wa kuona nafasi, kupenya ngome za wapinzani, na kutoa pasi zenye uzito ndicho kinachowatofautisha watoa asisti bora NBC Premier League 2024/2025 na wengine.
Vinara wa Assist NBC Premier League 2024/2025?
Mpaka sasa, Feisal Salum wa Azam FC na Pacome Zouzoua wa Young Africans wapo kileleni kwa utoaji wa assist msimu huu. Takwimu hizi zinasasishwa mara kwa mara kadri mechi zinavyoendelea.
Hii hapa orodha kamili ya watoa asisti bora hadi sasa:
Nafasi | Mchezaji | Timu | Utaifa | Asisti |
---|---|---|---|---|
1 | Feisal Salum | Azam | Tanzania | 13 |
2 | Pacome Zouzoua | Young Africans | Ivory Coast | 9 |
3 | Max Nzengeli | Young Africans | DR Congo | 8 |
4 | Prince Dube | Young Africans | Zimbabwe | 8 |
5 | Ki Stephane Aziz | Young Africans | Burkina Faso | 7 |
6 | Jean Ahoua | Simba | Ivory Coast | 7 |
7 | Josephat Bada | Singida BS | Ivory Coast | 7 |
8 | Salum Kihimbwa | Fountain Gate | Tanzania | 5 |
9 | Ismail Mgunda | Mashujaa | Tanzania | 4 |
10 | Marouf Tchakei | Singida BS | Togo | 4 |
11 | Iddi Kipagwile | Dodoma Jiji | Tanzania | 4 |
12 | Mohamed Hussein | Simba | Tanzania | 4 |
13 | Heritier Makambo | Tabora UTD | DR Congo | 4 |
14 | Iddy Selemani | Azam | Tanzania | 4 |
15 | Mudathir Yahya | Young Africans | Tanzania | 4 |
Angalia Hapa: Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025
Be the first to comment