
Katika moja ya mechi za kusisimua zaidi kwenye soka la Tanzania,(simba vs singida today) Simba SC itakabiliana na Singida Big Stars kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA Cup) mwaka 2025. Mechi hii itachezwa kwenye uwanja wa Kwaraha Stadium siku ya kesho tarehe 31/05/2025, na itahudhuriwa na mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia burudani safi ya soka la Bongo.
Historia ya Mikutano ya Simba vs Singida Big Stars
Timu hizi zimekutana mara kadhaa katika mashindano mbalimbali. Katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika Mei 28, 2025, Simba SC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Big Stars, bao pekee likifungwa na Steven Mukwala dakika ya 43
Simba vs singida big stars lineups
Kikosi cha Simba SC
Simba SC, chini ya kocha wao Fadru Davis, watakuja wakiwa na matumaini makubwa ya kufuzu fainali na kutwaa kombe hilo baada ya kupita misimu kadhaa bila mafanikio kwenye FA Cup. Kikosi chao kiliongozwa na nyota kama:
- Camarra
- Kapombe
- Mohammed Hussein
- Abdurazak Hamza
- Chamou Karaboue
- Yusuph Kagoma
- Joshua Mutale
- Fabrice Ngoma
- Steven Mukwala
- Charles Ahoua
- Elie Mpanzu
Kikosi cha Singida Big Stars
Singida Big Stars nao sio wa kubezwa. Watakuja na ari kubwa ya kutaka kushangaza, wakiwa na safu imara ya ulinzi na mashambulizi makali. Wachezaji kama:
- Arthur Bada – kiungo mwenye uwezo wa kupiga pasi za mwisho
- Elvis Rupia – mshambuliaji mwenye nguvu na uwezo wa kumalizia
Angalia Hapa: Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025
Be the first to comment