
Leo, Jumatano tarehe 28 Mei 2025, klabu ya Simba S C itamenyana na Singida Black Stars katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League).
Mahali na Muda wa Mechi
- Uwanja: KMC Complex, Dar es Salaam
- Muda wa Kuanza: Saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)
Historia ya Mikutano ya Timu Hizi
Simba S C na Singida Black Stars wamekutana mara 6 katika mashindano mbalimbali. Simba SC imeshinda mechi 4, huku mechi 2 zikiisha kwa sare. Singida Black Stars bado haijapata ushindi dhidi ya Simba SC. Katika mechi yao ya mwisho mnamo Desemba 28, 2024, Simba S C ilishinda kwa bao 1-0 ugenini
Kikosi cha Simba vs Singida Black Stars Leo
Simba SC:
- Mousa Camarra (Kipa)
- Kameta Duchu
- Valentine Nouma
- Che Malone
- Chamou Karaboue
- Yusuph Kagoma
- Joshua Mutale
- Debora Fernandez
- Leonel Ateba
- Jean Charles Aouha
- Elie Mpanzu
Angalia hapa: Msimamo Ligi Kuu NBC Tanzania 2024/2025
Singida Black Stars:
- Metacha (Kipa)
- Mkumbo
- Malonga
- Assinki
- Trabi
- Damaro
- Keyekey
- Pokou
- Adebayor
- Bada
- Sowah
Kumbuka: Vikosi hivi vinavyotarajiwa vinaweza kubadilika kulingana na maamuzi ya benchi la ufundi na hali za wachezaji kabla ya mechi.
Mahali pa Kuangalia Mechi
Mechi hii itarushwa moja kwa moja kupitia Azam Sports HD kwa watazamaji wa Tanzania, Kenya, Uganda, na Malawi.
Matarajio ya Mechi
Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 69 baada ya mechi 26, wakati Singida Black Stars inashika nafasi ya nne na pointi 53 baada ya mechi 27 . Kwa rekodi hii, Simba SC inaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kushinda mechi hii, lakini Singida Black Stars pia ina uwezo wa kutoa ushindani mkali.
Tegemea mechi ya ushindani mkubwa leo jioni!
Be the first to comment